Namuunga mkono Kigwangalla kwenye hili la DART

Namuunga mkono Kigwangalla kwenye hili la DART

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nakubaliana na Kigwangalla kwenye hili. Tatizo letu kubwa kwenye mradi huu ni wizi wa viongozi wa mradi.

Je wanaibaje? Viongozi wanaojinufaisha na mradi huu hawataki kata kata utumiaji wa kadi za mabasi ufanikiwe kwasababu ukifanikiwa hawataweza kuiba. Hivyo kila siku wana hakikisha kuna hitilafu kwenye mabasi kutumia card za nauli ili abiria walazimike kulipa cash pekee. Hivyo hakuna namna nzuri ya kujua ni watu wangapi au kiasi gani kimepatikana

Imefika wakati tumeshidwa hili kiasi kwamba viongozi wanaona kutatua tatizo ni luleta kampuni ya nje !

Hizi kampuni hazitafanya chochote cha ajabu zaidi ya kulazimisha (1) kila abiria anatumia kadi za nauli (2) Mtambo wa kadi unafanya kazi muda wote. Hiyo mitambo haina hitilafu yeyote maana wenzetu wanatumia hiyo hiyo mitandao na kadi na nchi nyingine hawajawahi kupata hizi hitilafu kwa miaka na miaka. Yaani tamaa kiasi kwamba hatuwezi kuendesha chochote

Attachments

  • F5944B6D-F609-4110-A541-A4757F8A9472.jpeg
    F5944B6D-F609-4110-A541-A4757F8A9472.jpeg
    46.6 KB · Views: 1
Kwa hapa tunajadili hoja yake muhimu. Tutoe mawazo yetu huwezi kujali kila mtu anasema nini.
Kwani Mkuu wa Mkoa na Waziri husika na usafirishaji wako wapi??
Huu ndio uzembe hasa katika nchi! Mapato yapo mnangangania Tozo!
Wizi wizi kila Kona!!!
 
Kwani Mkuu wa Mkoa na Waziri husika na usafirishaji wako wapi??
Huu ndio uzembe hasa katika nchi! Mapato yapo mnangangania Tozo!
Wizi wizi kila Kona!!!

Kabla hata ya mkuu wa mkoa hao wakurugenzi wanafanya nini? Au hata kama ni kampuni binafsi kwanini tusitafute kampuni za hapahapa!
 
Tatizo la mwendokasi sio mfumo wa kadi au mfumo wa nauli. Kigamboni Kuna mfumo wa kadi muda mrefu tu Ila nayo washashindwa.

Tatizo ni uwezo wa kusimamia mradi kutoka kwa management.

ATCL ilikufa sio kwa sababu watu wanalipa cash, ni utawala mbovu wa shirika.

NHIF mfumo wa malipo hata huwezi kujua Ila bado inapata hasara na tumeshindwa kufanya vizuri.

Tatizo nj management tu.
 
Kabla hata ya mkuu wa mkoa hao wakurugenzi wanafanya nini? Au hata kama ni kampuni binafsi kwanini tusitafute kampuni za hapahapa!
Na kwanini yasiwe makampuni ya nje ? Mbona madini wamepewa kuchimba makampuni ya nje ??!! Mimi hapa nikiwa na pesa za kutosha na nikataka kuinvest marekani mpaka Uraia watanipa !! Kama wenyewe tumeshindwa kujisimamia basi wapewe wa nje tusubiri kodi zetu tu !!
 
Tatizo la mwendokasi sio mfumo wa kadi au mfumo wa nauli. Kigamboni Kuna mfumo wa kadi muda mrefu tu Ila nayo washashindwa.

Tatizo ni uwezo wa kusimamia mradi kutoka kwa management.

ATCL ilikufa sio kwa sababu watu wanalipa cash, ni utawala mbovu wa shirika.

NHIF mfumo wa malipo hata huwezi kujua Ila bado inapata hasara na tumeshindwa kufanya vizuri.

Tatizo nj management tu.
Nini kifanyike mkuu maana kulaumu sio njia ya kutatua tatizo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lilianza pale walipoleta masuala ya nepotism kwa kumpa mamlaka kada mwenzao wa ccm ndugu kisena aendeshe mradi bila kujali km ana uwezo au vipi! Ilipaswa iitishwe tenda kampuni yenye vigezo zaidi ndio ishinde.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Tumeshindwa mangapi tumeua mangapi kuendelea kurudia yale yale kutegemea matokeo tofauti ni uchizi.
 
Back
Top Bottom