Nanauka: Madereva Bodaboda, Bajaji wamepatiwa nafasi 300 za kazi, Dubai

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema kwamba Rais Samia, katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyohidi kutafuta fursa za ajira nje ya nchi, tayari ameanza kutekeleza ahadi hiyo, ambapo waendesha pikipiki na bajaji 300 wanapelekwa Dubai kwa ajili ya kufanya kazi udereva wa bodaboda.

Amesema mikataba saba tayari imesainiwa na Serikali ili kufanikisha uwezeshaji wa watanzania kupata kazi nje ya Nchi.

Kwahiyo kama raisi akili yake ya kufikiri imeishia hapo?
 
Dubai..unashtukia uko Russia vitani mstari wa mbele..shoboka uone
 
Kwahiyo kama raisi akili yake imeishia hapo?
si huwa tunalalamika nje kuna wakenya wengi sana , kuna wanaigeria wengi sana wanapiga kazi? diaspora zao zinatuma sana hela kurudi nchini mwao?
 
Kwahyo ndio ajira alizoahidi samuya ndani ya siku 100.
Unadharau hizo kazi? Kwani una kisomo gani?

Wakenya wakutosha wanafanya kazi Emirates na Qatar Air, nyinyi bado mnataka muuze mitumba uwanja wa Karume??
 
Dereva bajaji au bodaboda anaenda kuendesha nini Dubai?! Au kuna kazi nyingine wanaenda kufanya kama cheap labour?
Cheap labour kwa Dubai inalipa kuliko graduate wa Tz.

Nashairi vijana changamkieni fursa hizo, achaneni na hawa pingpinga
 
300 out of millions ni sawa na tone moja baharini
Si haba hata hao 300. What if wasingepata huoni wangeongeza takwimu za unemployment Tanzania??

Je huoni pia diaspora remittance watakayoleta kwa kuwatumia ndugu zao hela kutoka huko?

Think outside the box and appreciate every effort irrespective how negligible it is.
 
Cheap labour kwa Dubai inalipa kuliko graduate wa Tz.

Nashairi vijana changamkieni fursa hizo, achaneni na hawa pingpinga
Mkuu acha masihara kabisa. Wanaenda kufanya kazi gani? Unajua lazima kuwe na agent anayepiganisha mtu kati?! Unadhani boda wote ni proffessional drivers?! Nanauka aweke wazi wanaenda kufanya kazi gani?! Huyo graduate unayemlinganisha na cheap labour wa Dubai ni yupi?
 
Kuna institutions za Serikali zinawafanyia testing. Kwa mfano mwaka jana madreva wa magari makubwa walifanyiwa test pale NIT ta kuendesha automatic trucks.

Ondoeni negativity ya hizi issues, gaya mambo yanaeezekana.

Mfano Philippines inaongoza kwa pato la diaspora (diaspora remittances) kutokana na wahudumu wa hoteli, maduka na majumbani bila kusahau na air hostesses wanaofanya kazi UAE.

Serikali ya Philippines ilipoiona fursa hii iliamua kufungua chuo kwa ajili ya ku train wahudumu wa sekta zote hizo
 
Kwa hiyo unaona bora wakae vijiweni wakicheza draft kuliko kuchangmkia fursa?? Mbona waNepal, Bangladesh na nchi zingine za Asia wako wamejaa Dubai wanajenga
Za kuambiwa changanya na za kwako...
 
Kuna institutions za Serikali zinawafanyia testing. Kwa mfano mwaka jana madreva wa magari makubwa walifanyiwa test pale NIT ta kuendesha automatic trucks.

Ondoeni negativity ya hizi issues, gaya mambo yanaeezekana.

Mfano Philippines inaongoza kwa pato la diaspora (diaspora remittances) kutokana na wahudumu wa hoteli, maduka na majumbani bila kusahau na air hostesses wanaofanya kazi UAE.

Serikali ya Philippines ilipoiona fursa hii iliamua kufungua chuo kwa ajili ya ku train wahudumu wa sekta zote hizo
Hakuna mtu mwenye negativity Mkuu. Haya mambo hayako wazi au tufanye mtoa taarifa kaleta taarifa haijakamilika. Nilikua na mwana msaidia mizigo wageni airport Dubai, almost ten yrs karudi home anafanya mambo yake. Hii ya kutuambia umechukua boda boda ni kama unaangalia group flani litalovutia kusikilizwa. Kwani kwa shida za bongo kuna graduate atakataa kwenda dubai? Kwa rumba la bongo graduate akatae kwenda Dubai kufanya kazii yoyote? Lazima wapo watakao kwenda, ila ukisema boda boda habari itauza zaidi, Kama kuwaita maafisa usafirishaji. Weka ajira wazi uone kama graduate hawatazichangamkia
 
Nimekuelewa
 
Back
Top Bottom