Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NANCY NYALUSI ATOA MAPENDEKEZO KWENYE BAJETI YA WIZARA YA KILIMO BUNGENI JIJINI DODOMA
"Wananchi wa Mkoa wa Iringa Tunaishukuru Serikali sana kwa mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Parachichi katika Wilaya ya Mufindi Kata ya Nyololo. Tunaomba Waziri atuambie ni lini ujenzi utaanza" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Iringa
"Tunaishukuru Serikali kwa ruzuku ya Mbolea, Wananchi wamefurahia sana. Tunaishukuru Serikali kwa kuweka ruzuku katika mbolea kwa wakulima mwaka 2023. Lakini msimu uliopita kulikuwa na changamoto ambazo zilitokea'" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Iringa
"Tunaomba mbolea zifike kwa wakati kabla msimu haujaanza kwa sababu mwaka 2022 mbolea ya kupandia ilichelewa hadi Mahindi yameshaota mbolea ya kupandia ndiyo inafika ambayo ilileta usumbufu mkubwa kwa wananchi na kero kubwa sana" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Iringa
"Tunaomba viwekwe vituo (Centre) ambavyo wakulima wataweza kupata mbolea kwa wepesi. Mfano, Iringa, mwananchi anatoka Mauninga karibia Kilomita 100 anafuata mbolea Iringa Mjini. Mwananchi anatoka Maduma anaenda mpaka Mafinga Mjini ndiyo apate mbolea, ni mateso makubwa sana" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Iringa
"Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, tunaomba mfumo wa ugawaji wa mbolea uendane na uhalisia wa maisha ya watanzania" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Tunaomba Mheshimiwa Waziri uanze zoezi la kusajili wakulima mapema kwa sababu suala la usajili siyo dharura. Unaweza kuanza kuwasajili sasa hivi ili kuondoa usumbufu ambao ulikuwa unajitokeza" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Pendekezo lingine ni Mamlaka ya Mbolea Tanzania 🇹🇿 mfumo wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania Tunaomba Mheshimiwa Waziri ukaufanyie mapitio una mapungufu mengi ambayo Mawakala wanailalamikia ili kuwaondolea mzigo Mawakala" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa
"Serikali ina mpango wa kuingiza zao la Mahindi kwenye mfumo wa Stakabadhi Ghalani katika Mikoa ya Nyanda Juu Kusini. Waziri atuambie amejipangaje maana tumeona kwenye zao la Choroko na Dengu kulikuwa na usumbufu mkubwa na changamoto nyingi kwa sababu wakulima wanahofu na wanataka kuondolewa hofu ili wawe na faraja katika jitihada zao za uzalishaji" - Mhe. Nancy Nyalusi, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa.