Nando wa BBA mbioni kutoa kitabu chake

Nando wa BBA mbioni kutoa kitabu chake

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindalo la Big Brother Africa The Chase, Ammy Nando anatarajia kutoa kitabu chenye kiitwacho ‘Mhuni Mwenye Akili.

Mhuni huyo Mwenye Akili' alitolewa kwenye shindano hilo baada ya kumtishia kumchoma kisu mshiriki mwenzake kutoka Ghana.

"Nando Wa Big Brother Africa kutoa kitabu chake cha pekee kitakacho toka kwa awamu mbili " English Version"na " Swahili Version.

Cha kiswahili ndicho kitakuwa cha kwanza kuchapishwa, Kitafahamika kwa jina la "MUHUNI MWENYE AKILI'," ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
 
Wai hamna muhuni mwenye akili zaidi ya kufanya upuuzi tangu atoke BBA kafanya nini
 
huyu jamaa u celeb wake ushachuja bwana, hana jipya tena.
 
Teheee.. Me naona tu warumi asijitese kwa kuleta habari zake tena humu maana sio celeb tena.. Kafulia, hana jipya,..u celeb wa 'one hit wonder' unaumbuaje...!!

utaniaribia kibarua, hao ma underground wananitafuta sana niwapaishe humu si unajua tena kupozwa na hela ya soda(joking) ahahaaa ahaha
 
Last edited by a moderator:
Hihihi Huyu tahira kweli kweli mi ni some hicho kitabu nami nianze kutembea na visu
 
Afu kama kiteja hiki kijamaa na anatoka na dayna nyange yule msanii wa muziki alieimba nivute kwako
 
Mpeni sapoti jamani ndyo nini kumkatisha tamaa Ivo....kijana Wa watu maskini ameamua kutafuta kipato chake kihalali bila yakumkaba mtu wala kumtapeli anachopata ni maneno ya dharau na kumpondea badilikeni jamani
 
Mxxxxxx ...hata kiuzwe sh 100/= sinunui

AHaha binamu bhana unanifurisha wewe kila bidhaa za mastaa hununui, sabuni ya mo yenye sura ya jokate hutaki , kitabu cha nando nacho umesema hata mia hununui
 
Afu kama kiteja hiki kijamaa na anatoka na dayna nyange yule msanii wa muziki alieimba nivute kwako

Ukaribu wao nadhan ulikuwa wa kikazi maana nimemuona nando kwenye video ya nyange
 
Alihojiwa huyo mdada kwene siz kitaa ya clouds tv akaulizwa akajiminya mwishowe akaeleza wazi kuwa ni baby wake
 
Back
Top Bottom