Nandy anazidi kupotea

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066


Hali ya Nandy kwenye muziki sio nzuri kwa kweli anahitaji sana support yetu. Haya mambo ya kushika keyboard na kumpa sifa za uongo hatumsaidii tumwambie ukweli graph yake inazidi kwenda chini siku baada ya siku.

Huyu sio yule nandy wa ninogeshe au kivuruge.

Nandy amefikia kufanya wimbo na Koffi na hasipate walau watazamaji million 1 ndani ya siku tatu sasa na amekaa namba moja trend kwa masaa hayazidi 8 akatolewa na habari.

Imagine uwekezaji wa million 70 unaishia kupata likes na comments za insta na JF inasikitisha sana. Huko kwenye platforms za downloads na streams ndio huruma kabisa.

Kwa mwendo huu mtawalaumu bure WCB kuwa ndio chanzo cha kushuka kwake.

Mtamlaumu Zuchu kwa kubeba attention za watoto wa kike ambazo awali zilikuwa kwa Nandy.

Wale mnaokujaga na magazeti ya kufarijiana msaidieni hata mawazo.

Siku si nyingi nitashusha uzi kama huu kwa yule kijeba anaejaribu kujinasua wakati mtumbwi ushazama.
 
Kijeba anaejaribu jujinasua nimecheka balaa ni nan uyo kijeba harmonize au !!!!
 
WATU HAMKUJUA WAKATI NANDY ANAACHIA AUDIO YAKE NA KOFFI NA WCB NAO WAKAACHIA SCANDAL YA RAY NA PAULO WATU WAKKACHA KUONGELEA NANDY NA KOFII IKAWA RAY NA PAULO HATA HII VIDEO HAIWEZI KUSAIDIA KITU KWASABABU AUDIO HAIKUFA CHOCHOTE
 
Unachosema hakina uhalisia kwasababu Nandy hajawahi kuwa na number kubwa za views youtube lakini nyimbo zake zipo mtaani. Nandy mi siku zote namuona anategemea radio na tv kuliko mitandao ya kijamii kupush nyimbo zake.
 
Misukule ya Domo At Work.

Mtoto Nandy lazima awalaze na viatu nyie MANYUMBU ya DOMOKAYA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…