Kwa wale mlioko Mwanza; kama ikiwezekana tufanye mpango tuonane viwanja vya Nyamhongoro ambako maonesho mbalimbali yanaendelea. Kwa jana nilienda na kujifunza mengi lakini kubwa zaidi ni kilimo cha Mihogo na namna ya kusindika products mbalimbali toka kwenye mihogo.
Leo nitakuwepo tena na nitaendelea kujifunza mengi ila ningependa kama nitakutana na memba wa JF tukabadilishana mawazo!
Panda magari yanayoenda kisesa, wambie wakushushe nane nane, hapo ndo penyewe, jiji limehamia hapo kwa wiki nzima, tupo tunajifunza, tunakula, tunakunywa n.k