Phonex Mpya
Senior Member
- Jun 21, 2025
- 128
- 39
Serikali imejenga na kukarabati zaidi ya masoko 50 na maghala 360 ya kuhifadhi mazao. Vilevile, imeanzisha vituo zaidi ya 30 vya huduma za pamoja (One Stop Centers) vinavyotoa pembejeo, ushauri, mikopo na masoko kupitia agrodealers 1,200 waliopo karibu na wakulima vijijini. Miundombinu hii imepunguza kwa kiasi kikubwa upotevu wa mazao baada ya mavuno, uliokuwa ukifikia hadi asilimia 30 hadi 40, na kuongeza bei za mazao mashambani kwa wastani wa asilimia 15 hadi 25, kwa mujibu wa NBS na TADB.
Hatua hizi zimeongeza tija, kuimarisha mnyororo wa thamani, kukuza biashara ya kilimo, na kuvutia uwekezaji kutoka sekta binafsi. Zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania hutegemea kilimo, hivyo uwekezaji huu ni kichocheo muhimu cha maendeleo endelevu ya Taifa.
Rais Samia ameanzisha vituo vya huduma ya kilimo ya Pamoja (One Stop Centers) kupunguza usumbufu na muda kwa sisi wakulima.