Asante Sana mkuu.Mimi ni mtu mzima. Nilikuwa kijana miaka ya mwanzoni mwa 2000. Nimejaribu kujiajiri, kuajiri na kuajiriwa. Naweza kusema kuna matatizo katika kila nyanja...kuanzia malezi, mazingira (sera) na mitaji.
1. Kwanza unapoongelea vijana inabidi uwagawe katika makundi matatu...kundi la kwanza ninwale wanaoishi elimu ya msingi au hawamalizi kabisa elimu ya msingi. Kundi la pili ninwale wanaomaliza elimu ya kati (form 4 au 6). Kundi la pili ninwale wanaohitimu vyuo (diploma/ degree). Haya makundi yana mahitaji tofauti na yana takiwa yawe treated tofauti. Kuwaweka vijana wote katika kapu moja ndo mwanzo wa kushindwa kutatua changamoto.za ajira.
Kundi la kwanza ni vijana ambao wanarudi kufanya shughuli za kiuchumi.zinazopatikana katika maeneo yao. Kwa mfano kama kuna machimbo wataenda kuchimba, kama kuna ziwa au bahari wataenda kuvua samaki na kama kuna mifugo wataanza kufuga....na kilimo.
Kwenye biashara hawa mara nyingi wanakuwa wachuuzi. Wachukue bidhaa sehemu A wauze sehemu B.
Kinacho wakwamisha vijana kwenye kundi hili ni ukosefu wa elimu za kazi wanazofanya. Wanavua samaki bila kiwa ana elimu ya uvuvi, wanalima bila kuwa na elimu ya kilimo n.k. Hivyo hujikuta hawana tija.
Kinachotakiwa hapa ni elimu juu ya kazi wanazozifanya. Bahati mbaya hakuna vyuo ambavyo vipo kwa ajili yao..ukiacha vyuo vya vyeta ambavyo vimejikita kwenye skills fulani fulani kama ujenzi, uashi, ufundi umeme n.k.
Tunahitaji kuwa na vyuo vya kila fani kutokana na shughuli za kiuchumi katika maeneo husika. Kwa mfano kama tungekuwa na vyuo vya uvivi kanda ya ziwa...acha kile cha nyegezi ambacho kinachukua watu wachache...ili kila mtu anaye vua awe na elimu ya uvuvi, kila anaye lima nyanya awe na elimu ya kuzalisha nyanya, kila.anaye lima mahindi awe na elimu ya kuzalisha mahindi Ili watu wasifanye kazi kwa mazoea ambazo hazina tija.
2. Vijana wa elimu ya kati...hawa mara nyingi wanatakiwa kuwa kama wa kundi la kwanza au kuwa ma supervisor. Hawa nao wanahitaji elimu kama kundi la kwanza ili wawasimamie au waajiri kundi la kwanza.
3. Vijana wa elimu ya juu hawa tatizo lao kubwa ni mfumo wa elimu. Wanamaliza wakiwa na vyeti lakini hawajui kazi walizosomea. Unakuta mtu ana vyeti say vya degree ya business administration halafu unamuuliza anaweza kufanya nini...hakuna. Hawa mara nyingi wanaandaliwa kuajiriwa na kupata additional on job training ndo wanaweza kufanya kitu.
Kwa hiyo kujaribu kutaka kundi hili wajiajiri kwa fani zao mara baada ya kuhitimu ni kitu ambacho hakiwezekani. Maana wanahitaji additional training ili kuwafanya wawe na fani. Elimu ya vyuo ni kama ya ku wa expose tu kwenye mambo mengi bila kuwajengea specific proffession. Hawawezi kujiajiri kamwe.
Therefore
1. Serikali na wadau wanahitaji kujenga kuwa na njia za kuwapa ujuzi watu wa kundi la kwanza na la pili.
2. Serikali inahitaji kuwapa incentive wataalamu ili waanzishe biashara ambazo zitaajiri watu wa kundi la tatu. Ni rahisi kwa mtu aliyekuwa kwenye ajira kwa miaka 10 kuanzisha biashara ambayo itaajiri vijana 20 kuliko kuwapa hela kikundi cha vijana 20 kuanzisha biashara. Hivyo basi naamini kabisa kama tunge twist sera kidogo tu..badala ya kutenge fedha kwa vikundi vya vijana katika halmashauri kama inavyofanyika sasa hivi na kusema watu wenye experience ya 10+ wapeleke mapendekezo ya miradi ya biashara wapewe fedha na waajiri vijana 10+ tatizo la ajira lingepungua sana.
Wahitimu wa chuo mara nyingi wanajiingiza kwenye uchuuzi badala ya kuzalisha. Hatuwezi kujenga uchumi.kwa kila mtu akiwa mchuuzi. Tutajenga uchumi.kama tutazalisha products ili tupunguze products tunazoagiza nje ya nchi na kuongeza products tunazo export. Hili haliwezi kufanywa na vijana wanaohitimu, ila watu wenye experience...wawezeshwe kuajairi vijana.
Mitaji bado ni tatizo kwa watu wazima wengi ambao wana mawazo na idea nzuri za uzalishaji.
So my advice is tu invest kwa watu wazima experinced proffesionals ili waajiri vijana wa makundi yote matatu
shukrani mkuu
kwel mkuu aslimia kubwa ndo hivo.Uvivu nishida na TamaaKwenye kujiajiri ni kutokufikiria zaidi na kufanya uchunguzi wa nini ambacho anaweza kukipeleka sokoni kikakubalika kirahisi.
Ila Mkuu tuache siasa nyingi pia
UVIVU TUU! na TAMAA za kijinga..
tukirudi kwenye kuajiriwa utakubaliana na mimi kuwa kila taasisi inahitaji watu wakugrow value ya shirika/kampuni sasa miongoni mwa vijana wengi wamejawa na uvivu + tamaa za haraka haraka anataka akipata hela tayari break yake ya kwanza kwenye gari na mademu! + MALEZI MABOVU.
Siku zote ukitaka kupima Inteligence test ya kijana mpe kazi bila pesa,hata ya kujitolea utaona vituko.
Mara hii wengi wanatamani wakipata kazi tuu wanavuta SUBARU na kuanza kusumbua mtaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna Theory nisizozipenda kama za kufanya unachipenda, ni penda unachofanya sio fanya unachopenda.Mimi ninadhani tatizo ni kwamba vijana tuna mawazo yanayorandana, mfano ukiona flani kafanikiwa kwa kulima nawe unataka kulima. Je una passion ya kuwa mkulima?
Katika maisha nimegundua utafanikiwa zaidi hasa ukianza na kitu unachokipenda toka moyoni kikawa ndiyo chanzo cha kukufunguliwa milango mingine.
Mimi sikuwahi kuajiliwa moja kwa moja na kampuni wala taasisi yoyote. Lakini imenichukua muda kugeuza kile ninachopenda kuwa pesa kwasababu sikujua nitawezaje kumonetize ninachopenda kuwa pesa mpaka ilipofika 2018.
Nashukuru kwasasa ninaona mwanga na kwakuwa nafanya kitu ninachopenda hata nikikutana na magumu siachi na ninaona baada ya miaka kadhaa nitakuwa mbali sana.
Tatizo siyo mtaji, tatizo ni kujua wataka nini na kufuata ndoto zako...
Hakuna Theory nisizozipenda kama za kufanya unachipenda, ni penda unachofanya sio fanya unachopenda.
Yes!