Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.
Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao
Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?
Sent using
Jamii Forums mobile app
SABABU KUBWA NI
MINDSET
Asilimia kubwa ya vijana mfano hapa Tanzania tunaishi chini ya utamaduni na mfumo wa maisha unaofanana kwa wengi. Kutokana na hali hii, wazazi/walezi wanaandaa vijana kusoma ili wapate kazi nzuri kwa kuajiriwa. Hvyo kijana anaanza kusoma akilenga kuajiriwa sehemu fulani na sio kujiajiri sehemu fulani. Kutokana na % kubwa kuwa na Mindset inayofanana, ndiyo maana tatizo la ukosefu wa ajira linazidi kuwa kubwa kwa vijana wengi.
SABABU BAADHI NDOGO NDOGO ZINAZOUNDA SABABU KUBWA TAJWA HAPO JUU NI-:
1. Kijana Kutotambua wapi aanzie ili kujiajili.
2. Vijana wengi wanahisi hawana uwezo wa kufanya kazi fulani wakisema kazi hzo ni za watu fulani au ni za mataifa fulani na mwisho wa siku hukaa bila kuwa na kitu cha kufanya maana kila wanachofikiri wanaona kwao hakiwezekani.
3. Uzembe wa kuchukua hatua, yaani kijana anasema kesho nitafanya na kesho huzaa kesho bila kuanza anachokifikiri.
4. Kukosa plan B na hvyo Kupoteza muda mwingi kulaumu Serikali, ndugu na marafiki badala ya kuangalia nini cha kufanya.
5. Vijana wengi wanahisi kujiajiri ni kuuza bidhaa tu na kama hana fedha za kuanzisha biashara fulani basi anakaa wakati anaweza kuanzisha biashara inayouza huduma na akaingiza fedha nyingi bila hata mtaji wa fedha.
6. Baadhi walijaribu kujiajiri lakini walichagua mawazo ya biashara yasiyosahihi (WRONG BUSINESS MODELS) ambapo biashara zao zilikufa mapema na wakakata tamaa.
NINI KIFANYIKE KAMA SULUHU
Suluhu kubwa ya tatizo la ajira ni jamii kwa ujumla kubadili MINDSET zao ili mtu awe na mawazo ya kujiajiri tokea akiwa mdogo.
MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA KAMA SULUHU NI KAMA
1. Jambo la kwanza ni kuepuka vikwazo kama hivyo nilivyovitaja hapo juu.
2. Vijana watambue mtaji mkubwa ni akili na uwezo waliopewa na mwenyezi Mungu wala sio pesa.
3. Vijana wasiwe wabinafsi. Mfano, mtu anawazo zuri la biashara na hana pesa na anashindwa kumshirikisha mwenzake mwenye pesa ili waanzishe biashara na hivyo anakaa na wazo lake hadi linakufa bila mafanikio.
4. Vijana wasikimbilie kuuliza biashara gani inalipa wataangukia shimoni maana mahesabu ya kwenye karatasi ni tofauti na mahesabau halisia. Hivyo vijana wajikite katika kutatua matatizo ya watu hapo ndipo kuna biashara inayolipa maana mtu akitatuliwa tatizo lake yuko tayari kulipa kiasi chochote.
5. Kila kijana aamini kuwa anauwezo wa kufanya jambo fulani hata kama anahisi hana uwezo wa kufanya. Imani inaweza kufanya mambo makubwa.