Nani adui wa vijana katika Kujiajiri. Ni Uthubutu, Serikali, au Malezi na Mazingira?

Uthubutu na Serikali ndio tatizo. Ninaposema serikali na maanisha mazingira wezeshi. Hata hivyo kunahitajika utafiti ili kujua mzizi hasa wa tatizo hili. Tunachofanya hapa ni opinions na sio fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi tatizo kubwa ni serikali

Serikali haijaweza kujipanga kuwajenga vijana wajitegemee. (Mtoto umleavo ndivo akuwavo)

1. Serikali haina sera bora kuwajenga vijana

2. Serikali haijawa namikakati bora na kabambe kuwajengea vijana uwezo kujiajili
A. Elimu yetu mtaala wa hovyo.... nadhalia kwa wingi vitendo yaani practicals zero

B. Mazingira
- mitaji sahihi sio hela nyanya kuhadaa vijana Visenti vya kulimia robo heka bila mbolea wala madawa imeisha

- Karakana wezeshi zenye vifaa vyote ilikuboresha ujuzi na maarifa ya vijana

- uhamasishaji sahihi, sio mapambio yakisiasa na ulaghai mitaani katika kulenga kupigiwa kura

- masoko ya bidhaa, serikali inapaswa kuona mbali na kupanga mipango ya makusudi kitaalamu sio kisiasa. Ili vijana iliowaanda kimkakati katika sera bora wajiendeleze kwa miradi yao.

Nk nk nk

Dhana ya vijana wachache kutoka yaani mmoja mmoja kufanikiwa haiwezi kuwa utetezi ama sababu kuwabeza au kuwaona duni waliowengi ambao hawana lakufanya

Ukichimba kwa kina hao mmoja mmoja waliofanikiwa utakuta lazima pembeni kuna aliyesaidia kwa namna moja ama nyingine wakajijenga. (Huwa hawasemi ukweli halisi kwa 100% walivofanikiwa)
Baba
Ndugu
Rafiki
Au mfadhili

Bila ya
1. Mtaji sahihi
2. Mazingira bora
3. Elimu .....sio lazima ya darasani... (uelewa wa jambo alifanyalo kwa undani iwe kilimo, biashara nk.)

Hapa ndipo tunakwama.

unaweza kuwa na vyote bila mtaji, bila mazingira bora (sera na mipango ya serikali sahihi) hatutatoka milele

muwe na mjadala mwema 🙌🙌🙌
 
Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.

Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao

Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Malezi mabovu toka kwenye familia zetu, utakuta mzazi anajua kuajiliwa ndiyo mpango mzima, mtu anayejiajili wanasema ameshindwa shule.

Ukoloni: ulidumaza wengi wakajua kuajiliwa na mzungu au serikali ndiyo mpango mzima { white color job}

Mazingira: Serikali siyo rafiki kwa wafanyabiashara wao walioajiliwa na serikali (wanasiasa, TRA, BRELA, na taasisi zingine wanajua wafanyabiashara ni watu wa kuhujumu uchumi, hivyo ukianzisha biashara ni kama unaanzisha mugogoro na serikali)

Akili mbovu za vijana wengi kuwa na aibu na uthubutu kufanya shughuli za kujitegemea.
 
Kwangu mimi tatizo kubwa ni serikali

Serikali haijaweza kujipanga kuwajenga vijana wajitegemee. (Mtoto umleavo ndivo akuwavo)

1. Serikali haina sera bora kuwajenga vijana

2. Serikali haijawa namikakati bora na kabambe kuwajengea vijana uwezo kujiajili
A. Elimu yetu mtaala wa hovyo.... nadhalia kwa wingi vitendo yaani practicals zero

B. Mazingira
- mitaji sahihi sio hela nyanya kuhadaa vijana Visenti vya kulimia robo heka bila mbolea wala madawa imeisha

- Karakana wezeshi zenye vifaa vyote ilikuboresha ujuzi na maarifa ya vijana

- uhamasishaji sahihi, sio mapambio yakisiasa na ulaghai mitaani katika kulenga kupigiwa kura

- masoko ya bidhaa, serikali inapaswa kuona mbali na kupanga mipango ya makusudi kitaalamu sio kisiasa. Ili vijana iliowaanda kimkakati katika sera bora wajiendeleze kwa miradi yao.

Nk nk nk

Dhana ya vijana wachache kutoka yaani mmoja mmoja kufanikiwa haiwezi kuwa utetezi ama sababu kuwabeza au kuwaona duni waliowengi ambao hawana lakufanya

Ukichimba kwa kina hao mmoja mmoja waliofanikiwa utakuta lazima pembeni kuna aliyesaidia kwa namna moja ama nyingine wakajijenga. (Huwa hawasemi ukweli halisi kwa 100% walivofanikiwa)
Baba
Ndugu
Rafiki
Au mfadhili

Bila ya
1. Mtaji sahihi
2. Mazingira bora
3. Elimu .....sio lazima ya darasani... (uelewa wa jambo alifanyalo kwa undani iwe kilimo, biashara nk.)

Hapa ndipo tunakwama.

unaweza kuwa na vyote bila mtaji, bila mazingira bora (sera na mipango ya serikali sahihi) hatutatoka milele

muwe na mjadala mwema [emoji119][emoji119][emoji119]

Ayo yote yanaweza kuwa kweli lkn the bottom line ni kwamba uchumi wa tanzania ni mdogo sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndio maana tunataka mawazo yako mkuu
Kama hayo yote sio tatizo
Tatizo ni nini?
1. Aibu...... nikweli nchi nzima vijana wanakwama sababu wanaaibu? Sio kweli

2. Uzembe .... nikweli vijana mikoa yote wazembe? Sio kweli

3. Elimu.... nikweli vijana wakitanzania asilimia kubwa Elimu haiwasaidii .... may be but not certainly

4. Malezi.... nikweli malezi yanawakwamisha maelfu ya vijana! Kwamba wazazi wanamalezi yakufanana nchi nzima? Kigoma, tanga, mtwara .... singida......shinyanga? Sio kweli

5. Mazingira... je mazingira yanaweza kuwa sababu? May be but not certainly kwa taifa zima

6. Uthubutu.... nikweli vijana wengi hawana uthubutu? Kivipi kama taifa tunaongelea asilimia kubwa ya vijana zaidi ya 50%

7. Uoga... kwamba zaidi ya 50% ya vijana wetu waoga? Sio kweli

Kipi cha kweli sasa, ama nini mtazamo wako?
 
Mimi nilijaribu kufanya kautafiti kidogo
Sample yangu ilikuwa vijana 50 kutoka mikoa miwili tofauti

42 kati yao walisema tatizo ni mtaji

5 Walisema Sera mbovu za serikali hasa kwenye kutafuta masoko ya nje kwa bidhaa zinazozalishwa Tanzania ( hasa kilimo)

2 Walisema mazingira na jamii uliyokulia inakushape mmoja alinipa mfano wa life style ya Wahaya vs Wakinga na Wachagga

1 Aliniambia yeye anauwezo wa kupata mtaji lakini hajui aanzie wapi, afanye bishara gani (Hana elimu ya biashara na fedha)
Kuna kitu kinaitwa root cause failure analysis (RCA)

bila ufaham mzuri kila mtu atazuka na visababu vyake kimtazamo ambavyo sio root cause.

lakini jibu sahihi lisilenge mtu mmoja ametokaje Bali asilimia mfano 50% au 70%

tunapotoa majibu tunatakiwa kutazama Wastani wa wahusika sio mafanikio ya mtu mmoja watatu au wanne sababu hawa hawawakilishi sample spaces or representative sample

vijana kwanini asilimia kubwa hawawezi kutoka/kufanikiwa/kupiga hatua/kujiajiri/kujitegemea/kujijenga ...... tatizo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haiwezekani tatizo la vijana maelufu kushindwa kuwa ni :-

1. Aibu

2. Uzembe

3. Elimu

4. Malezi

5. Mazingira

6. Uthubutu

7. Uoga

Nk
Haiwezekani mamilioni wanateseka lazima kunatatizo la msingi ambalo ni common yaani Root cause
Root cause ni lack of creativity
 
Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.

Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao

Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo...
""WANAOPIGA KELELE VIJANA TUJIAJIRI WOTEE WAO WAMEAJIRIWA""

#YNWA

Wrote from Anfield..!!
 
WATEJA.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Wakuu,
Poleni na majukumu ya kila siku.

Katika ulimwengu wa sasa ambapo watu wenye taaluma mbalimbali wamejikuta mitaani bila kuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, ningependa kupata maoni yenu na pengine suluhu ya vijana kujiajiri na kuajiri wenzao

Nini hasa kikwazo kinachowafanya vijana wengi washindwe kujiajiri
Ni Sera, malezi, Aibu, Mazingira au Uthubutu?

Sent using Jamii Forums mobile app

SABABU KUBWA NI MINDSET

Asilimia kubwa ya vijana mfano hapa Tanzania tunaishi chini ya utamaduni na mfumo wa maisha unaofanana kwa wengi. Kutokana na hali hii, wazazi/walezi wanaandaa vijana kusoma ili wapate kazi nzuri kwa kuajiriwa. Hvyo kijana anaanza kusoma akilenga kuajiriwa sehemu fulani na sio kujiajiri sehemu fulani. Kutokana na % kubwa kuwa na Mindset inayofanana, ndiyo maana tatizo la ukosefu wa ajira linazidi kuwa kubwa kwa vijana wengi.

SABABU BAADHI NDOGO NDOGO ZINAZOUNDA SABABU KUBWA TAJWA HAPO JUU NI-:

1. Kijana Kutotambua wapi aanzie ili kujiajili.
2. Vijana wengi wanahisi hawana uwezo wa kufanya kazi fulani wakisema kazi hzo ni za watu fulani au ni za mataifa fulani na mwisho wa siku hukaa bila kuwa na kitu cha kufanya maana kila wanachofikiri wanaona kwao hakiwezekani.
3. Uzembe wa kuchukua hatua, yaani kijana anasema kesho nitafanya na kesho huzaa kesho bila kuanza anachokifikiri.
4. Kukosa plan B na hvyo Kupoteza muda mwingi kulaumu Serikali, ndugu na marafiki badala ya kuangalia nini cha kufanya.
5. Vijana wengi wanahisi kujiajiri ni kuuza bidhaa tu na kama hana fedha za kuanzisha biashara fulani basi anakaa wakati anaweza kuanzisha biashara inayouza huduma na akaingiza fedha nyingi bila hata mtaji wa fedha.
6. Baadhi walijaribu kujiajiri lakini walichagua mawazo ya biashara yasiyosahihi (WRONG BUSINESS MODELS) ambapo biashara zao zilikufa mapema na wakakata tamaa.

NINI KIFANYIKE KAMA SULUHU

Suluhu kubwa ya tatizo la ajira ni jamii kwa ujumla kubadili MINDSET zao ili mtu awe na mawazo ya kujiajiri tokea akiwa mdogo.

MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA KAMA SULUHU NI KAMA

1. Jambo la kwanza ni kuepuka vikwazo kama hivyo nilivyovitaja hapo juu.
2. Vijana watambue mtaji mkubwa ni akili na uwezo waliopewa na mwenyezi Mungu wala sio pesa.
3. Vijana wasiwe wabinafsi. Mfano, mtu anawazo zuri la biashara na hana pesa na anashindwa kumshirikisha mwenzake mwenye pesa ili waanzishe biashara na hivyo anakaa na wazo lake hadi linakufa bila mafanikio.
4. Vijana wasikimbilie kuuliza biashara gani inalipa wataangukia shimoni maana mahesabu ya kwenye karatasi ni tofauti na mahesabau halisia. Hivyo vijana wajikite katika kutatua matatizo ya watu hapo ndipo kuna biashara inayolipa maana mtu akitatuliwa tatizo lake yuko tayari kulipa kiasi chochote.
5. Kila kijana aamini kuwa anauwezo wa kufanya jambo fulani hata kama anahisi hana uwezo wa kufanya. Imani inaweza kufanya mambo makubwa.
 
Tatizo sio serikali, mtaji , malezi wala mazingira, Tatizo ni kukosa uhakika wa kuuza. Watu wengi wanapenda kufanya biashara Ila hawana uhakika wa kuuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa. Ila uhakika wa kuuza unakuja pale mtu anapoanzisha biashara bila kujua kama watu wanauhitaji wa bidhaa zake au huduma yake. Ila kama mtu akiuza bidhaa au huduma ambazo watu wako tayari kununua hawezi kosa wateja.
 
Bilashaka wewe ni muhenga mkuu

Umenena vyema Sana.
SABABU KUBWA NI MINDSET

Asilimia kubwa ya vijana mfano hapa Tanzania tunaishi chini ya utamaduni na mfumo wa maisha unaofanana kwa wengi. Kutokana na hali hii, wazazi/walezi wanaandaa vijana kusoma ili wapate kazi nzuri kwa kuajiriwa. Hvyo kijana anaanza kusoma akilenga kuajiriwa sehemu fulani na sio kujiajiri sehemu fulani. Kutokana na % kubwa kuwa na Mindset inayofanana, ndiyo maana tatizo la ukosefu wa ajira linazidi kuwa kubwa kwa vijana wengi.

SABABU BAADHI NDOGO NDOGO ZINAZOUNDA SABABU KUBWA TAJWA HAPO JUU NI-:

1. Kijana Kutotambua wapi aanzie ili kujiajili.
2. Vijana wengi wanahisi hawana uwezo wa kufanya kazi fulani wakisema kazi hzo ni za watu fulani au ni za mataifa fulani na mwisho wa siku hukaa bila kuwa na kitu cha kufanya maana kila wanachofikiri wanaona kwao hakiwezekani.
3. Uzembe wa kuchukua hatua, yaani kijana anasema kesho nitafanya na kesho huzaa kesho bila kuanza anachokifikiri.
4. Kukosa plan B na hvyo Kupoteza muda mwingi kulaumu Serikali, ndugu na marafiki badala ya kuangalia nini cha kufanya.
5. Vijana wengi wanahisi kujiajiri ni kuuza bidhaa tu na kama hana fedha za kuanzisha biashara fulani basi anakaa wakati anaweza kuanzisha biashara inayouza huduma na akaingiza fedha nyingi bila hata mtaji wa fedha.
6. Baadhi walijaribu kujiajiri lakini walichagua mawazo ya biashara yasiyosahihi (WRONG BUSINESS MODELS) ambapo biashara zao zilikufa mapema na wakakata tamaa.

NINI KIFANYIKE KAMA SULUHU

Suluhu kubwa ya tatizo la ajira ni jamii kwa ujumla kubadili MINDSET zao ili mtu awe na mawazo ya kujiajiri tokea akiwa mdogo.

MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA KAMA SULUHU NI KAMA

1. Jambo la kwanza ni kuepuka vikwazo kama hivyo nilivyovitaja hapo juu.
2. Vijana watambue mtaji mkubwa ni akili na uwezo waliopewa na mwenyezi Mungu wala sio pesa.
3. Vijana wasiwe wabinafsi. Mfano, mtu anawazo zuri la biashara na hana pesa na anashindwa kumshirikisha mwenzake mwenye pesa ili waanzishe biashara na hivyo anakaa na wazo lake hadi linakufa bila mafanikio.
4. Vijana wasikimbilie kuuliza biashara gani inalipa wataangukia shimoni maana mahesabu ya kwenye karatasi ni tofauti na mahesabau halisia. Hivyo vijana wajikite katika kutatua matatizo ya watu hapo ndipo kuna biashara inayolipa maana mtu akitatuliwa tatizo lake yuko tayari kulipa kiasi chochote.
5. Kila kijana aamini kuwa anauwezo wa kufanya jambo fulani hata kama anahisi hana uwezo wa kufanya. Imani inaweza kufanya mambo makubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapokuwa na tatizo kubwa.....

Tatizo lilitapakaa nchi nzima......

Tatizo la jamii nzima kwa maana ya asilimia...

Mhusika mkuu kulitatua ......?! SERIKALI PEKEE. IKIFANYA UJINGA INAJENGA TAIFA LA WAJINGA. (Japo wapo wachache wataibuka)

Tatizo lakitaifa hutatuliwa kitaifa kwa maamuzi ya

1. kisera,
2. usimamizi
3. na mafunzo ya kitaifa.

nje ya hapo nikujidanganya
 
Back
Top Bottom