Nani akinusuru Chuo cha Ualimu Korogwe?

Nani akinusuru Chuo cha Ualimu Korogwe?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Wazalendo


Chuo cha Ualimu Korogwe


S.L.P. 533, Korogwe


NDUGU Mhariri,
Sisi ni watumishi wazalendo katika Chuo cha Ualimu Korogwe, mkoani Tanga. Tunasikitishwa na uendeshaji mbovu wa chuo chetu.
Uongozi wa juu wa chuo umekuwa dhaifu katika kuchukua uamuzi wa kiutawala ili kulinda hadhi ya chuo hiki kitaifa na kimataifa. Tumejitahidi bila mafanikio kukabili uzembe wa kiuongozi chuoni hapa.
Juhudi zetu ni pamoja kuripoti katika mamkala husika, ikiwamo ngazi ya wizara. Tunaamini kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha za chuo, kuanzia fedha za michango, miradi ya chuo na hata zile zinazoletwa chuoni kutoka wizarani.
Wapo wenzetu waliodiriki kuhoji hadharani, kumuandikia nyaraka mbalimbali na hata kushauri uongozi wa juu wa chuo bila mafanikio. Maarifa yote ya kiutaratibu na kikanuni yalifuatwa bila mafanikio na wengine ilibidi siku moja kumfungia mkuu wa chuo ofisini kama hatua ya kumshinikiza aondoe uozo chuoni.
Hatua zote hizo zimekuwa zikilenga kuwezesha mabadiliko ya kimfumo chuoni na kujibu hoja za msingi, ikiwamo kuitishwa kwa vikao vya ripoti za mapato na matumizi.
Athari za uongozi mbovu chuoni zimeanza kujitokeza ambazo ni pamoja na kuporomoka kwa kiwango cha taaluma chuoni. Kwa mfano, matokeo ya watahiniwa wa mtihani wa taifa kwa mwaka 2012 ni mabaya, zaidi ya watahiniwa 310 wanatakiwa kukariri masomo waliyofeli hapo mwakani wakati wenzao watakapokuwa wanafanya mtihani mingine, pia wapo wanachuo 67 waliofeli kabisa hivyo hawana sifa za kuwa walimu popote pale.
Gharama serikali inazoingia kumsomesha mwanachuo mmoja kwa miaka miwili si chini ya milioni sita (ukijumuisha mishahara ya watumishi, na gharama nyingine za uendeshaji).
Wakufunzi wamekuwa wakiomba vikao vya kujadili hali ya kitaaluma, kwa mfano, kujadili matokeo hayo mabovu lakini kutokana na maovu ya uongozi, imekuwa vigumu vikao hivyo kufanyika.
Tunaamini vikao haviitishwi kwa sababu uongozi utabanwa kuhusu mwenendo wake mbovu. Kero mbalimbali zimekithiri chuoni, kuanzia hali duni ya maktaba ambayo huchangiwa Sh. 10,000 na kila mwanachuo tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi leo lakini hali ya jengo la maktaba si ya kuridhisha.
Hakuna vitabu vya kutosha maktaba, chumba cha maktaba kilichopo hali yake ni mbaya, maabara ya kompyuta si ya kuridhisha. Kuna madai kwamba fedha zinazotoka wizarani kwa ajili ya ukarabati zimekuwa zikitafunwa sambamba na fedha za michango ya Sh. 10,000 kila mwaka ya wanafunzi.
Mashine za kudurufu ni tatizo, wino kwa ajili ya mashine hizo hakuna na wanafunzi hujigharimia ili angalau kujitafutia elimu bora. Inafikia mahali hata barua za mkuu wa chuo zinakaa kwa karani wake zaidi ya wiki mbili bila kuchapwa kisa eti wino hakuna! Hii ni aibu kwa chuo kikubwa kama hiki.
Ndugu mhariri, chuo kina miradi na huduma kadhaa ambazo ni sehemu ya vyanzo vya mapato bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini. Baadhi ya vyanzo vya mapato vya chuo ni pamoja na fedha zinazotokana na huduma ya chakula kupitia mradi wa “Domestic Science” (DS).
Mradi huu unaendeshwa zaidi wakati wa kazi mbalimbali maalumu zinazofanyika eneo la chuo, kwa mfano shughuli za Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) au shughuli nyingine kama semina.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa inayokiingizia chuo fedha nyingi lakini hali ya chuo haiendani na mamilioni ya shilingi yanayopatikana kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Upo mradi wa mnara wa simu, mradi mdogo wa kantini ya chakula, mradi wa huduma ya mafunzo ya muda mfupi kwa wanafunzi wa sekondari maarufu kwa jina la TAI (Teachers Academic Initiatives) na wale wa elimu ya awali ambao nao unaingiza fedha. Tunaamini mapato ya miradi hii hayafanani na taarifa zilizopo na kwa kweli tunashangazwa na wakaguzi wa hesabu wanaofika chuo hapa na kuondoka kimya kimya bila kuwapo na ripoti kuhusu hali halisi.
Chuo chetu kimepoteza mvuto kwa sababu ya uongozi mbovu, miaka ya nyuma chuo kilikuwa kikipokea wanafunzi zaidi ya 1500 lakini leo hii hata 200 ni vigumu kuwapata. Wakati mwingine tunadhani ni njama zinazohusisha hata vyuo binafsi ili wanafunzi wakasome huko badala ya chuo hiki chenye sifa ya kipekee nchini.
Haturidhiki na mbinu zinazotumiwa na uongozi wa chuo katika kukabili matatizo haya kwa sababu uongozi ni sehemu ya matatizo haya.
Uongozi wenye tuhuma katika miradi ya chuo ukiwamo mradi wa majoho kwa ajili ya mahafali ya wanachuo haupaswi kuaminika kuongoza chuo cha kitaaluma, tena taaluma nyeti ya ualimu. Uongozi unaojihusisha na michango ya fedha za wanafunzi katika hali ya shaka kubwa haupaswi kuongoza chuo hiki.


 
mh.mulugo atakuwa ameipata hiyo subirini utekelezaji wake, hilo ni jembe hata kama alitelezesha ulimi south.
 
Msijali, Serikali yetu ni sikivu na tayari tushaunda tume kuchunguza madai yenu,hata hivyo ndio maana tunawapa nafasi nyingi za upendeleo za kusahihisha mitihani ili mjiingizie kipato!
 
Mulugo alikuwa huko Korogwe juzi mbona hakupita huko chuoni?
 
Mulugo alikuwa huko Korogwe juzi mbona hakupita huko chuoni?

Alipita mkuu, ameeelezwa uhalisia wote, ameongea na wakufunzi na nasikia kuna maamuzi magumu ameyafanya kiasi kuna baadhi ya walimu/wakufunzi walilia hadharani.
 
huo mchango wa maktaba naona una kaharufu ka ufisadi hela zachangwa tu bila maendeleo yeyote
 
Awamu hii taasisi nyingi hazipati fedha ya kutosha,usishangae matatizo yapo kwenye Tasisi kama hii.Mambo mengi hayafanyiki kwa uwazi katika kuzihudumia taasisi zilizo chini ya wizara ya Elimu,hii ni kwa sababu ya Ubinafsi,na kutokuwa na nia ya dhati ya kuwasilisha na kushughulikia matatizo yaliyo katika Sekta hii ya Elimu.

Usishangae,walimu wanaandaliwa hapa,bado wakifika sehemu za kazi bado wanakutana na matatizo ya kiutumishi,kimasilahi na mazingira ya kazi yasiyoboreshwa.!!
Tatizo ni Wizara yenyewe,kushindwa kusimamia,kulinda na kutetea maslahi ya Taasisi,na watumishi katika sekta hii.

 
Hicho chuo ni cha kibiashara sana afu wizi nje nje me nimemaliza hapo mwaka 2006 nimerudi mwaka huu kuchukua cheti yaani nilitaman kulia sio kocet ninayoifahamu. Afu wakufunzi wa pale hawafundishi kabisa wanajali biashara zao tu inakuaje watu wengi namna hiyo wafeli. Wizara lazima itume wakaguzi wa ufundishaji na mahesabu
 
Macho na nguvu zimeelekezwa Elimu ya juu (vyuo vikuu). Hivyo vyuo baadaye kidogo.
 
Maamuzi yalishafanyika. Mkuu wa chuo alihamishwa chuo nakushushwa cheo, wakufunzi wengine wamehamishwa na kushushwa vyeo tofauti walivyohodhi awali. Sasa chuo kipo shwari. Hongera kwa serikali kulifanyia kazi hili
 
Back
Top Bottom