Nani aliipa jina la 'Taifa Stars' timu yetu? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,822
Wakuu hiki jina Taifa stars nani aliipa timu yetu yaTaifa? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?
Ninadhani kunapokuwa na mafanikio kwa timu ya Taifa ni fursa pia ya kutangaza alama maalumu ya Taifa ambayo bila shaka inaweza chochea pia utambulisho wetu na utalii wetu.

Mfano Uganda wanajiita the crane.
Bila shaka wakimaanisha ndege adimu wanaopatikana kwa wingi Uganda.

Wengine wanajiita "mamba weusi"
Wengine "Tai wa Jangwani"
Wengine "simba wa theranga"
Hapo jirani nadhani kwa sabbu ya machimbo ya shaba wanajiita "risasi za moto" chipolopolo.
Ama kule kusini wanajiita "Bafana bafana"

Je kwanini timu yetu ya Taifa isiwe na utambulisho maalumu wenye kuleta maana?

Mfano tukaiita timu yetu "the giraffe"..
"Tukiamini kuwa twiga ni mnyama anayekula majani ya juu ya miti."

Na anaeona Mbali zaidi adui yake kabla hajamkaribia. Pia Twiga ni kimbilio kwa wanyama wengi wasio weza kumuona adui yao kwa mbali..

Napendekeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa Miguu iitwa "THE GIRAFFE "!
 
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.
 
Mi napendekeza iitwe the Hyena,yaani fisi,itatufaa sana,yaani sisi huwa tunaqualify kwa ubest luza tu,hakuna siku tunaongoza group yaani ni kama fisi kula mizoga tu na ni muoga vby,juzi tulikua cape verde watu wamejipigia 3:0
 
Kongole mkuu haya ndiyo mawazo stahiki hii ni timu yetu sote.
Pia jina huelezea Mengi sana kuhusu nyie mnaoitwa hivyo. Au mnaotumia jina hilo..
 
Mi napendekeza iitwe the Hyena,yaani fisi,itatufaa sana,yaani sisi huwa tunaqualify kwa ubest luza tu,hakuna siku tunaongoza group yaani ni kama fisi kula mizoga tu na ni muoga vby,juzi tulikua cape verde watu wamejipigia 3:0
Hapa duniani kuna roho mbili zinazoongoza nafsi roho mbaya. Na roho nzuri. Sabbu wewe umeamua kuitwa FISI ni vema wewe na ukoo wako mkaitwa hivyo lakini sisi wengine tunatazama kwa mtazamo ulio chanya zaidi.
Ndio maana tunahitaji mabadiriko ya jina ambalo litabeba maana kwa Taifa letu.
"TANZANIA."
 
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.
Mleta Uzi anazungumzia ALIAS za Timu, mf hao ENGLAND ni THREE LIONS! Sa anashangaa why Tanzania alias Taifa Stars na sio THE GIRAFFE au THE TANZANITE, hivyo yaani!
 
Naunga mkono hoja

Siungi mkono jina pendekezwa la twiga, ni mpole na ni victim kama walivyo nyumbu tu

Bora hata angeitwa Serengeti, halafu wale watoto watafutiwe jina lingine
 
Wazee wa viswahili pale CHUO CHA DAR
Mkuu Mkiki. Una historia yoyote ya utoaji wa hilo jina "Taifa stars" ututupie hapa? Lakini pia kama walikuwa wazee wa kiswahili nadhani neno "stars" linatengeneza ukakasi kwenye kiswahili.
 
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.
England - The Three Lion

Brazil - Selecao

Hao wengine pia wana majina yao japo sijayakariri

Wote hao wana majina yanayobeba tukio/maliasili/jambo linalotambulisha nchi husika
 
Naunga mkono hoja

Siungi mkono jina pendekezwa la twiga, ni mpole na ni victim kama walivyo nyumbu tu

Bora hata angeitwa Serengeti, halafu wale watoto watafutiwe jina lingine
Mkuu elezea kuhusu serengeti. Ama ingeitwa "the Tanzanite"!
 
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.

Na kwamba hiyo stars inatia kaukakasi kidogo, kana vimelea vya ugeni, ni wakati sasa kutukuza kiswahili
 
Hii nchi imejengwa kwa misingi ya uchawi, ushirikana, wanga na nguvu za Giza. Kitu kama Mwenge kililetwa na Forojo Ganze a.k.a Master bingwa wa uchawi ili watz wawe mapoyoyo na manyumbu watawalike kirahisi.
Sitaona ajabu kuwa Kuna kigagula mmoja ndiye aliyependekeza jina la Taifa Stars.
Miongoni mwa matokeo ya Mwenge ni kulala kwa huzuni ndio maana miradi mingi na vitu vingi chini ya chama cha Mwenge na serikali havina matokeo chanya
 
Umaanisha ndio maana hata soka letu kama Taifa halisogei mbele!
 
Naunga mkono hoja ya kuwa na jina lenye maana ya kuitangaza nchi.
Ila binafsi napendekeza iitwe eitha:
-THE LIONS PRIDE, lions pride ni kundi la simba wanaoishi kama ukoo, wanalindana dhidi ya maadui ma wanashirikiana ktk kutnza ukoo. Au
-THE WILD DOGS. Hawa mbwa mwitu inapokuja suala la timu work achana nao. Kwa ushirikiano wao wanaweza muangusha mnyama/ adui mkubwa na kummaliza kwa kumla kabla hata ajafa. Yaani wanamla akiwa mzima.

Jina la nickname inapendeza linakuwa linatangaza kitu tulichonacho na pia linatisha. Hawa ni wanyama ambao tunao mbugani mwetu.
 
Hivi kuna uwezekano wa kuongea masuala mengine yasiyo ya kisiasa bila kuweka siasa?
Huu ni utaahira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…