Nani aliipa jina la 'Taifa Stars' timu yetu? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?

Nani aliipa jina la 'Taifa Stars' timu yetu? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?

Wakuu hiki jina Taifa stars nani aliipa timu yetu yaTaifa? Linabeba ama kutangaza kitu gani kwa Nchi yetu?
Ninadhani kunapokuwa na mafanikio kwa timu ya Taifa ni fursa pia ya kutangaza alama maalumu ya Taifa ambayo bila shaka inaweza chochea pia utambulisho wetu na utalii wetu.

Mfano Uganda wanajiita the crane.
Bila shaka wakimaanisha ndege adimu wanaopatikana kwa wingi Uganda.

Wengine wanajiita "mamba weusi"
Wengine "Tai wa Jangwani"
Wengine "simba wa theranga"
Hapo jirani nadhani kwa sabbu ya machimbo ya shaba wanajiita "risasi za moto" chipolopolo.
Ama kule kusini wanajiita "Bafana bafana"

Je kwanini timu yetu ya Taifa isiwe na utambulisho maalumu wenye kuleta maana?

Mfano tukaiita timu yetu "the giraffe"..
"Tukiamini kuwa twiga ni mnyama anayekula majani ya juu ya miti."

Na anaeona Mbali zaidi adui yake kabla hajamkaribia. Pia Twiga ni kimbilio kwa wanyama wengi wasio weza kumuona adui yao kwa mbali..

Napendekeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa Miguu iitwa "THE GIRAFFE "!
Jina liitwe 'Burigi-Chato Stars'
 
England ni "three lions" hao wengine sijui.
JAPO NAKILI SIJUI nickname ZAO ILA wenzetu wanatimu zao zinaitwa
ENGLAND
SPAIN
BELGIUM
BRAZIL
CROATIA
KWANINI TUSIJIITE TU TANZANIA? KAMA LINAUKAKASI KULINGANA NA MUUNDO WA MUUNGANO WETU BASI WATAFUTE JINA JINGINE NA SIO MAMBO YA WANYAMA.
 
Majina hayana effects yoyote kiufundi au kiuwezo uwanjani

Mpira ni technics na uongozi mzuri, majina ni kitambulisho au nembo tu.
 
Hivi kuna uwezekano wa kuongea masuala mengine yasiyo ya kisiasa bila kuweka siasa?
Huu ni utaahira.

TAIFA ni sawa kwani linawakilisha uniqueness kwa ushahidi wa utaifa wenye nguvu(ukilinganisha na nchi zingine zenye ukabila n.kj). Ni kwa kuwa hatuja perform vizuri tu otherwise jina bado zuri.
 
Back
Top Bottom