Nilimsindikiza mtu kuapply kazi ila nikaishia kuipata mimi kazi.
Jamaa haelewi mpaka leo anahisi nilimzunguka ila ni Mungu tu alinipangia iwe rizki yangu.
Wakati jamaa kaingia ndani kupeleka application yake mimi nilibaki nje nikimsubiri.
Kulikuwa na watu wawili wanaongea kwenye parking karibu ya nilipokuwa nimekaa.
Katika maongezi yao walikuwa wanaelekezana sehemu ambapo ilibidi mmoja wao aende na taxi. Kutokana na kutozungumza kwao kiswahili ikawa tabu kuelekeza dereva wa taxi.
Walipotaka kuita mmoja wa waajiriwa wa kampuni, nilijitolea tu kumuelekeza dereva wa taxi maana toka mwanzo nilikuwa nasikia maongezi yao.
Baada ya huyo mmoja kuondoka aliebaki akaanza kunihoji nasubiri nini pale. Nikamwambia ninachosubiri.
Aliuliza nafanya kazi gani, nikamjibu sina kazi ndio kwanza nimemaliza kusoma.
Alinipa business card yake na kutaka siku ya pili niende na cv yangu.
Jamaa yangu alipotoka alikuta ndio namalizia maongezi na huyo mtu ambae nilikuja kugundua ni director wa hiyo kampuni.
Nilipomwambia jamaa yangu kilichotokea alibadilika hapo hapo na kununa. Aliitisha bodaboda na kuondoka.
Siku ya pili nilipeleka CV yangu na siku hiyo hiyo kupata ajira.