Nani alikuwa msanii wa kwanza wa Bongo fleva?

pitbull

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
596
Reaction score
184
Naomba kujunzwa tafadhali, msanii ambaye alikua wa kwanza kuimba mziki wa Bongo fleva.
 
Saleh Jabr. Alitamba na vibao cha "ice ice baby" na mwingine sijui unaitwaje but alikuwa anatumia rythm na beat ya wimbo wa Chakka Demus & Plius wa "murder she wrote" hiyo ilikuwa ni early 90's

vp kuhusu cool james mtoto wa dandu..??
 
Salehe Jabir brother ake Salama Jabir ndiyo Msani wa kwanza wa Bongo flv
 
Shule bado hazijafunguliwa jamani ??
 
Saleh Jabir sio msanii wa kwanza wa bongo flavor,miondoko ya kurap ilikuwepo sema ilikuwa ya kiingereza sema Jabir alifanya kwa kiswahili.
 
Saleh Jabir sio msanii wa kwanza wa bongo flavor,miondoko ya kurap ilikuwepo sema ilikuwa ya kiingereza sema Jabir alifanya kwa kiswahili.

point yako ni nzuri ila swali ni muziki wa bongo fleva ni upi?
 
Saleh Jabir ni msanii wa kwanza kurekodi album ya rap kwa kiswahili hapa Tanzania ... Ila kujua msanii wa kwanza ni ngumu maana harakati zilianza kitambo mitaani kabla ya kuanza utaratibu wa matamasha kwenye mashule na baadae mashindano ya rap ....Harakati zilikuwepo hasa Dar, Morogoro, Mbeya, Tunduma na Arusha .....muziki huo kuitwa Bongo fleva ni baadae sana na neno lenyewe Bongo fleva lilianzishwa na producer Nguli P Funk Majani wa Bongo Record ....
 
point yako ni nzuri ila swali ni muziki wa bongo fleva ni upi?

P Funk ni producer mkali wa Rap (sipendi kutumia neno Hiphop hapo) na kipindi hicho alikuwa anarekodi rap tu ...hivyo mantiki yake itakuwa kuita Bongo fleva kwa vile ilikuwa ni rap ya kiswahili ikizungumzia mambo ya waswahili ....ila wasanii wa kuimba walivyoanza kuibuka wote na wa rap wakawa wanaitwa wasanii wa Bongo fleva hadi baadhi ya wasanii wa rap walipoamua kuanzisha harakati ya kujitofautisha na wasanii wa kuimba kwa kutaka wao waitwe wasanii wa Hip hop na si Bongo fleva ....
 
Na yule jamaa aliyeimba..."kalibuuzi kalibuzi langu kalichuna mimi na rafiki yangu,siku ya kwanza kivyanguvyangu,siku ya pili kivyanguvyangu,siku ya tatu na rafiki yangu"
 
Watu walikuwa wana-rap kwa kiswahili kabla ya Saleh Jabir. Ilikuwa kwenye matamasha katika kuiga style za wamerekani kulikuwa na ma-MC wanaoingiza vionjo vya kiswahili.
 
Uko sawa Mkuu,Nakumbuka Mr 2 ananyimbo yake Inaitwa Bongo flv, nakumbuka baadh ya maneno ktk ile nyimbo anasema...Albam ya kwanza nilipata laki mbili...albamu ya pili nilipata milioni mbili...ya tatu na ya nne tia akilili
 
Duh hao wengine me siwafahamu nnachokumbuka bongo fleva upande wa rap nimeanza kuisikia kwa kina Balozi, Kwanza unit, sugu na wengine na upande wa rnb na zouk walikwepo kina Mr Paul...nakumbuka nilikua primary enzi hizo!
 
Saleh Jabr. Alitamba na vibao cha "ice ice baby" na mwingine sijui unaitwaje but alikuwa anatumia rythm na beat ya wimbo wa Chakka Demus & Plius wa "murder she wrote" hiyo ilikuwa ni early 90's
Maelezo yako ya awali ni sahihi lakini Ice Ice Baby alitumia beat ya Vanilla Ice na wimbo wa Vanilla ulikuwa unaitwa hivyo hivyo... Ice Ice Baby!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hivi huyo unaemwongelea hapa Jabir saleh ni huyu mtangazaji wa Times Fm?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…