Nani alikuwa msanii wa kwanza wa Bongo fleva?

Nani alikuwa msanii wa kwanza wa Bongo fleva?

Mi nimeanza kusikia enzi ya Kina kwanza unit, Sugu, na wengine wala siwakumbuki ila ice ice baby ya kibongo pia naikumbuka japo sijui wimbo upi ulianza
 
Cj Massive, Cool James Mtoto wa Dandu. The founder of awards in TZ.

Hzo takataka nyingine cjui akina sos b na maandazi mengine hayapo kwenye Ramani.
 
Saleh Jabir ni msanii wa kwanza kurekodi album ya rap kwa kiswahili hapa Tanzania ... Ila kujua msanii wa kwanza ni ngumu maana harakati zilianza kitambo mitaani kabla ya kuanza utaratibu wa matamasha kwenye mashule na baadae mashindano ya rap ....Harakati zilikuwepo hasa Dar, Morogoro, Mbeya, Tunduma na Arusha .....muziki huo kuitwa Bongo fleva ni baadae sana na neno lenyewe Bongo fleva lilianzishwa na producer Nguli P Funk Majani wa Bongo Record ....

hahahahah tunduma lilikuwa pori mkuu
 
Saleh Jabbir, Marehemu Nigger One wa Kwanza Unit, Consumer hawa niliwasikia mwanzo kabisa....

Ki ukweli si rahisi kumfahamu muanzilishi wa bongo fleva kwani mtindo wao wa kufanya Rap walivuviwa na akina Mc Hammer na wengineo kutoka nje. Pia mtindo huu wa kufokafoka ulianza kupata umaarufu kupitia Bottles Parties, birthday parties na kuasisiwa vyema kupitia school parties bila kusahau Beach Parties.

Kuna historia kubwa ya mtindo huu wa muziki. Lakini haijawa tapped vizuri.
 
So far namkumbuka saleh jabir kabla yake sikumbuki. Ila baada ya saleh jabir namkumbuka hashim dogo, then wakaja kina diplomats, mawingu, KU, GWM, II proud etc
 
hahahahah tunduma lilikuwa pori mkuu

Sugu anajua vyema mchango wa Tunduma kwenye Hiphop enzi hizo ....Marehemu Fred Jebby wa Arusha alikuwa anakwenda Tunduma kukutana na wanaharakati wengine wa Hiphop na kushiriki matamasha ....ile boda ya kijanja sana na ukitaja maeneo yaliyokuwa na harakati hizo kitambo lazima Tunduma itajwe ....
 
Mkuu hivi huyo unaemwongelea hapa Jabir saleh ni huyu mtangazaji wa Times Fm?

Hapana, namzungumzia huyu .....

saleh-j.jpg
 
James Dandu alishuka TZ kutoka Sweden wakati Bongo Flavor imeshashika chat na watu wameshaachana na Umarekani!!

Hivi huu jamaa alitoa albamu moja alafu akakimbia, namkumbuka sana nyimbo zake zote zilikuwa nzuri zikibebwa na wimbo wa nakuhitaji. Enzi hzo nikiwa darasa la tano
 
Uko sawa Mkuu,Nakumbuka Mr 2 ananyimbo yake Inaitwa Bongo flv, nakumbuka baadh ya maneno ktk ile nyimbo anasema...Albam ya kwanza nilipata laki mbili...albamu ya pili nilipata milioni mbili...ya tatu na ya nne tia akilili

MC shika Mic mkononi
watu nyoosha mikono hewani...
bongo fleva...bongo flevaaa..

ilikuwa kwenye album ya ITIKADI hii!!
 
Uko sawa Mkuu,Nakumbuka Mr 2 ananyimbo yake Inaitwa Bongo flv, nakumbuka baadh ya maneno ktk ile nyimbo anasema...Albam ya kwanza nilipata laki mbili...albamu ya pili nilipata milioni mbili...ya tatu na ya nne tia akilili
Na ndy msani wa kwanza kununua gari pia! Nakumbuka ilikuwa model ya Honda

Ovaaa
 
Kama sio Nikki Mbishi basi atakuwa One Incredible
 
kuna mtu anaitwa SAREH JABIR alikuwa anatafsir nyimbo za mbele kama za wakina SHABBA RANKS,nakumbuka ilikuwa mwaka 94 au 95 hv.
 
John Dilinga Maclaw "the legend" akiwa RadioOne, alikuwa na kipindi cha usiku alikiita "bongo flavor" na ndio ilikuwa Radio ya kwanza na Presenter wa kwanza kuurasmisha mziki huu, kwa kuupeleka Radioni na pia kuubatiza. Na akaenda mbali zaidi baadae, kwa kumbatiza Joseph Haule "Profesa"
 
Back
Top Bottom