JK AZINDUA KITABU CHA SIR GEORGE KAHAMA
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akizindua kitabu kinachohusu Historia ya Maisha ya Utumishi Serikalini cha Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kutoka kushoto wanaoshuhudia ni Rais Mstaafu Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama (wapili kushoto), Rais Mstaafu Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (wanne kushoto) na watano kushoto ni Mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Royalty, Bwana Joseph kahama.