Nani alitunga Sheria ya Usalama Barabarani?

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Sijui ni lini tutakuwa serious kama nchi.

Mimi sifuatiliagi sana vipengele vya kisheria ila hii nimejikuta naipitia kwa sababu zangu binafsi. Nimecheka japo inakera sana.

Sheria hii ya ajabu kwanza ilitungwa kabla ya Katiba ya mwaka 1977. Yenyewe ilitungwa 1973. Nadhani ilitungwa na wakoloni. Hawa jamaa walikuwa walevi sana.

Haiwezekani sheria hii iweke ukomo wa kilevi kuwa ni 0.08g/dl aisee. Hapa ni kuruhusu madereva kuendesha roho za watu au mali wakiwa bwiii! Matokeo take ndio hizi ajali zisizoeleweka.

WHO yenyewe inaeleza kuwa dereva mwenye kiwango hicho cha ulevi anakua hatarini kupata ajali mara nne zaidi ya yule ambaye hajatumia pombe kabisa.

Bora tungefuata ushauri wa WHO kuwa ukomo wa ulevi uwe ni 0.05g/dl kwa madereva wazoefu na 0.02g/dl kwa madereva wapya wasio na uzoefu.

Pia sheria hii ni kama imewaacha salama walevi wanaotembea kwa miguu. Hawa hawana limit kabisa kisheria na wanavuka barabara. Fikiria!

Acha hilo la matingasi. Kuna wale jamaa wanaopiga misele mitaani kwa fujo. Unakuta gari imeachiwa spidi kitaa unabaki kushika mdomo. Kuna watoto wanabutuliwa kila siku.

Haya yote tunaweza kusema ni ajali na uzembe. Sawa. Adhabu zake zinatosha kukomesha? Kichekesho.

Dereva mwenye leseni faini yake haizidi laki moja kwa makosa yote ya barabarani, hata akigonga na kuua. Mlevi anayetembea kwa miguu hana faini kabisa.

Haya mapitio ya Sheria hii yaliyofanywa mwaka 2002 yalirekebisha nini sasa?

Kwangu mie nimeona hayo. Najua humu kuna wataalamu watanielekeza kisheria ni vipi tunaweza kupata marekebisho mapya yapelekwe bungeni kama mapendekezo. Angalau kupitia mtandao tutakuwa tutakuwa tumewasaidia hawa jamaa kutunga Sheria inayoeleweka.

Karibuni mawakili na wanasheria wasomi mtudadavulie!
 
Niliwahi kukamatwa kwa kosa la mtembea kwa miguu na kupigwa faini isiyonihusu.

Na hapo nilikuwa najaribu kumkwepa vile alikuwa anavuka barabarani akiwa amelewa.

Hakuna siku niliyochukia kama hiyo. Hizi sheria zinapaswa zikate kotekote!

Halafu, adhabu tunazonyooshwa na matrafiki barabarani unaona hazitoshi? Sio dereva wewe.
 
Ilikuwa mitaa gani
 
Huo nao ni udhaifu mwingine wa sheria hii. Ndio maana nikataka wasomi watusaidie.

Jiweke kwenye nafasi tofauti na udereva halafu angalia kwa mfano hizi adhabu na makosa yake


1. KUSABABISHA MADHARA KWA MWILI AU KIFO KUPITIA UENDESHAJI WA HATARI. KIF.40
Kosa hili linamhusu mtu yeyote aliyemgonga mtu na kusababishia madhara au kumuua kutokana na uendeshaji wa gari kwa papara au kwa mwendokasi ambao kwa kuzingatia mazingira yay a eneo husika, mwendo huo ni hatari kwa umma au kwa mtu yeyote yule. Pia kosa hili linamhusu mtu yeyote anayesababisha madhara au kifo kutokana na kushindwa kulimudu gari kulikosababishwa na ulevi au matumizi ya madawa ya kulevya.

ADHABU
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa hili adhabu yake chini ya kifungu cha 63(2)(a) cha sheria ni kifungo kisichopungua miaka mitatu, na kwa kuongezea juu ya kifungo, faini isiyozidi shilingi laki moja. Kifungu hiki kinatumia neno “shall”kuonesha kuwa mahakama haina chaguo bali inalazimika kukufunga bila kukupa mbadala wa faini.

2. KUSABABISHA MADHARA KWA MWILI AU KIFO KWA UZEMBE(KUTOJALI) KINYUME NA KIF.41

Kosa hili linamhusu mtu yeyote anayesababisha madhara kwa mwili au kifo kwa uzembe/ kuendesha gari bila kuchukua tahadhari au kuwa makini. Adhabu ya kosa hili inapatikana kifungu cha 63.

ADHABU
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa hili adhabu yake chini ya kifungu cha 63(2)(b) cha sheria ni faini au kifungo jela kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano. Hapana utaona kwamba pamoja na sheria kutumia neno “shall”lakini mbele yake inaweka neno “or”ili kuipa mahakama uhuru wa kuamua kati ya kifungo na faini. Kwakuwa faini ndio inaanza basi mtuhumiwa atapewa kwanza chaguo la kulipa faini, akishindwa kifungo ndipo kitafuata.

3. UENDESHAJI WA PAPARA AU HATARI KINYUME NA KIF.42

Kosa hili linamhusu dereva ambaye akiwa barabarani anaendesha kwa pupa/papara au anaendesha gari kwa spidi ambayo kwa kuzingatia vigezo vyote spidi hiyo itakuwa ni hatari kwa umma au kwa mtu yeyote yule au kwa ujumla uendeshaji wake tu ni hatari.

Tofauti ya kosa hili na mawili ya hapo juu ni kwamba dereva anakuwa anaendesha kwa hatari au kwa papara lakini hasababisha madhara au kifo. Ila ni dereva rafu tu hata bila kutumia tochi. Hapa ushahidi wa kimazingira tu unatosha kuthibitisha hili.

ADHABU
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa hili adhabu yake chini ya kifungu cha 63(2)(b) cha sheria ni faini au kifungo jela kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano. Hapana utaona kwamba pamoja na sheria kutumia neno “shall”lakini mbele yake inaweka neno “or”ili kuipa mahakama uhuru wa kuamua kati ya kifungo na faini. Kwakuwa faini ndio inaanza basi mtuhumiwa atapewa kwanza chaguo la kulipa faini, akishindwa kifungo ndipo kitafuata.

4. KUZUIA MSAFARA.
Kifungu 43

Kosa hili linamhusu dereva ambaye ataingilia au kuzuia msafara. Kuzuia au kuingilia msafara ni pamoja na kutotii maelekezo ya askari anapoandaa njia ya msafara na msafara ukashindwa kupita, au msafara wakati unapita na wewe unachomeka gari lako, au kabla msafara haujapita unaegesha gari lako katikati ya barabara au hautaki kupisha.

ADHABU
Kwa kosa hili adhabu yake ni faini au kifungo kisichopungua miezi 12 na kisichozidi miaka 5.

5. KUENDESHA GARI UKIWA UMEZINGIRA NA ULEVI au MADAWA YA KULEVYA. KIF. 44

Hiki kifungu kinawahusu watumia tangawizi(wantumia vileo) wote, kiasi kwamba unashindwa kabisa kulimudu au kulicontrol gari. Tofauti ya kosa hili na linalofuata hapo chini ni moja tu; Kwamba chini ya kifungu hiki mtuhumiwa sio lazima apimwe na kukutwa amezidi kiwango cha 80mg/100mls. Kwa kosa hili inatosha kuthibitika kuwa kutokana na kutumia pombe umeshindwa kuendesha gari vizuri.

ADHABU
Mtu yeyote atakayetiwa hatiani kwa kosa hili adhabu yake chini ya kifungu cha 63(2)(b) cha sheria ni faini au kifungo jela kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano. Hapana utaona kwamba pamoja na sheria kutumia neno “shall”lakini mbele yake inaweka neno “or”ili kuipa mahakama uhuru wa kuamua kati ya kifungo na faini. Kwakuwa faini ndio inaanza basi mtuhumiwa atapewa kwanza chaguo la kulipa faini, akishindwa kifungo ndipo kitafuata.

6. KUKUTWA NA KILEVI ZAIDI YA KIWANGO KILICHOWEKWA. Kifungu 45

Kosa hili linahusu wale ambao kwenye dam zao kuna kiwango kikubwa cha pombe kinachozidi 80mg/100mls kwenye damu. Kiwango hiki kinathibitika baada ya kufanyiwa kipimo cha pumzi(breath test) au kipimo cha damu maabara au kwa kutumia alkometa.

ADHABU
Kama kiwango cha ulevi kitazidi 150mg katika 100mls za damu utapigwa faini au kifungo kisichopungua miaka miwili na kischozidi miaka mitano.

Iwapo kiwango cha ulevi kimevuka kiwango lakini 150mg katika 100mls za damu basi utapigwa faini au kifungo kisichopungua miaka miwili na kisichozidi miaka minne.
 
Ni kweli sheria hii inapaswa kurekebishwa kwa sehemu kubwa tu. Max speed kwa mujibu wa sheria hii ni 80 KPH, enzi hizo wkt sheria inatungwa baraba zailikua za vumbi na magari ni yale ma Leyland Albion na Fiat.

Sio sababu ya kubaki na mwendokasi huo enzi hizi hasa kwa gari ndogo. Lakini pia adhabu zinahusu wenye vyombo vya moto, hazihusu raia wasiofuata sheria za usalama barabarani kama kuvuka mahali pasipo na zebra.
 

Well said.

Yaani Sheria imemfanya mtembea kwa miguu kuwa mfalme, wakati wapo wengine madish yao yameyumba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…