GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
πππ nimecheka sana, siku hizi PhD ni sawa na elimu ya dara la saba tu kila mwanasiasa anayo, wao wenyewe wanafuraha sana kuitwa Dr. na hata hawaelewi uDr wao unatoa au unasaidiq nini jamiiAnyways kwakuwa sasa kwa Tanzania kama una Ndoto za kuja Rais wao basi Sharti ni lazima Umiliki PhD (Doctorate) iwe ya Academical au Honorary (ya Huruma, Utu na Upole) ili Uogopwe na Wapiga Kura.
Na Mimi GENTAMYCINE najipanga sasa Kuwaroga Watoa PhD's maarufu nchini UDOM na UDSM ili wajikute tu wananipa nami ili 2025 Jina langu katika Karatasi ya Kura lianze na Dkt. GENTAMYCINE na siyo GENTAMYCINE na ni matumaini yangu makubwa Watanzania mnaowaogopa wenye Doctorates na kuwaona ndiyo wana Akili na ni kila Kitu mtanipa Kura zenu za ndiyo kwa Uwingi na hatimaye kuwa Rais wenu ajaye na nawaahidi sitowaangusha Abadan.
Sisi tunataka maisha bora kwa kila mtanzania sio tuzo.Hizo tuzo mbona hazina uhusiano na maisha ya wabongo.Watanzania tujenge hoja Kama tunaoelewa mambo sio uchawa na unafiki tu.Hakuna mtu aliyebembeleza hao udsm and the likes..
Kama udsm wamebembeleza na Hawa waliotoa tuzo kadhaa kwake nao utasemaje?
Kapata tuzo ya miundombinu kutoka AfDB
Kapata tuzo ya Uongozi wa Kimageuzi ya Afrema,
Kapata tuzo ya Afya ya Care,
Kapata tuzo ya Mshikamano imetolewa na Kanisa,
Kapewa tuzo na Wasanii nk nk
Swali kote huko alimbembeleza Nani? Sasa kwa taarifa yako many more are coming joandae kisaikolojia wewe hater.