Nazikumbuka Tungo za R.O.M.A
"Uchafu wa Mrisho, unamfanya Benja aonekane msafi"
"We ni mkwere wa Chalinze ambae hautomsahau Mnyakyusa, Mwakyembee alowafunisha Monduli siasa"
"Wameacha tizi wakaoa ka Mrisho Ngasa, mi nakomba pesa zote nasepa kama Lowasa"
"Bandugu bwaga manyanga, ayaokote Magufuli"
Na nyingine nyingi unazozikumbuka hasa kwa msimu huu wa kuelekea 25/Oct
Je ni nini kilimsibu hadi kufikia ukimya huo?
Rudia kusoma ulichoandikaJapo lowasa fisadi kweli ila roma hana kipaji
Asante sana mkuu.Ukimya umekuja baada ya kujua uonevu na udhaifu wa CCM.
CCM ilimwangushia Lowassa zigo la Richmond ili kumwokoa Rais
Roma pamoja na Kalla wametambua ukweli pamoja nasi sote.
Ndio maana tunamtaka Lowassa kama alivyo!
Bandugu bwaga manyanga abaogote Magufuri...... Na ndio anayaokota kwel baada ya Oct....... Nakomba pesa zote kisha nasepa kama Lowasa Ahahahaha afu anataka ikulu..... Shame on you mnaoshikiwa akili.
Roma watu walichoka mziki wake wa kutabirika, mtu anakaa kimya mwakamzima na tunajua kabisa akirudi atarudi na muktasari wa matukio ya mwakamzima, sa yanini si bora nisikilize taarifa ya habari au nisome magazeti tu. Mwanamziki hautakiwi utabirike, Diamond ingawa anaimba mapenzi ila nyimbo zake ukisikiliza unaona kabisa zinatofautiana, ni ngumu pia kumtabiri mtu kama Joh Makini atakuja na kitu gani hata style ya flow anachange, but Roma vocal zake zote zinakaa kwenye beat moja
Ni kweli aisee, nimeona hata mapokeo ya hii track yake mpya. Bila kuhamia kwenye siasa za wazi ( kusapot upande mmoja) sidhani kama huu wimbo ungepata hata mtu wa kuuongelea. Sema anabebwa na vuguvugu la mabadiliko