Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kabla ya yote naomba kuwapa pole Wafanyabiashara wenzangu wa Kariakoo kwa kuangukiwa na jengo, nimeguswa moja kwa moja na ajali hii kwa sababu nina washirika wangu wa kibiashara wamepata janga, tumuombe Mungu awafanyie Wepesi, Amina.
Kwa kadri ya Umri nilio nao na kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kukumbuka kuona wala kusikia Mtumishi wa umma wa ngazi ya Chini kama RC akijifanyia ama akifanyiwa tathmini (ripoti) ya kipindi fulani cha uongozi wake (Niko Tayari kusahihishwa)
Sasa huko Arusha kuna jambo linaloendelea, kwamba eti Mtumishi wa Umma ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo ndugu Paulo Makonda anatoa ripoti ya Utumishi wake wa Umma kwa kipindi cha miezi 6 alichotumikia kazi hiyo!
Ripoti hiyo inatolewa ili iwe nini? kwanza imeandaliwa na Nani na kwanini? na baada ya ripoti hiyo kutolewa nini kitafuata?
Halafu kwanini ni Makonda tu na wala si Ma RC wengine?
Naomba mwenye majibu anisaidie