Pre GE2025 Nani ameandaa kinachoitwa Ripoti ya Miezi 6 ya Makonda? Kwanini na ili iweje?

Pre GE2025 Nani ameandaa kinachoitwa Ripoti ya Miezi 6 ya Makonda? Kwanini na ili iweje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jamaa ni mbunifu wa kazi na utekelezaji wake, sioni tatizo na hakuna aliekatazwa kuonesha mafanikio yale na mapungufu yake
 
kwa wasio na malengo na wasio na mipango mikakati hii itakua haina maana kwao..

But this gentleman, Paul Christian Makonda, Arusha RC, is a really visionary and modern leader of new era 🐒
Anatumia nyakati bara'bara!
 
Naona kama imekosa focus, badala ya kumjenga inataka kumfanyia mambo ya ghorofa la kariakoo
 
Itatuchukua miaka mingi sana kuirudisha nchi kwenye utawala wa sheria.
Magufuli katuachia mfumo ambao RC ana nguvu kuliko Waziri wa wizara fulani, mfumo ambao Dc ana nguvu kuliko mbunge au diwani.
 
Sijui kama anakosea....nadhani yeye jamaa huwa ana hulka ya kutaka kuwa tofauti na ma RC wenzie, pia kutopoa..kutofanya kwa mazoea, kutaka kuonekana...nk nk.. sabab nadhani ni kama hatakagi kuwa sawa nao walio nyanja moja...na hata kudharau mawaziri....hata alipokuwa Dar aliwahi kufanya mambo mengi ambayo yalikuwa sio kawaida ya MaRC kufanya na hata ikawa ndio kama kiranja wa MaRC wote nchi nzima..nadhani kimkakati , binafsi zaidi anajiongeza kwa mambo yajayo..muhimu kama havunji sheria.
 
Kabla ya yote naomba kuwapa pole Wafanyabiashara wenzangu wa Kariakoo kwa kuangukiwa na jengo, nimeguswa moja kwa moja na ajali hii kwa sababu nina washirika wangu wa kibiashara wamepata janga, tumuombe Mungu awafanyie Wepesi, Amina.

Kwa kadri ya Umri nilio nao na kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kukumbuka kuona wala kusikia Mtumishi wa umma wa ngazi ya Chini kama RC akijifanyia ama akifanyiwa tathmini (ripoti) ya kipindi fulani cha uongozi wake (Niko Tayari kusahihishwa)

Sasa huko Arusha kuna jambo linaloendelea, kwamba eti Mtumishi wa Umma ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo ndugu Paulo Makonda anatoa ripoti ya Utumishi wake wa Umma kwa kipindi cha miezi 6 alichotumikia kazi hiyo!

View attachment 3154582

Ripoti hiyo inatolewa ili iwe nini? kwanza imeandaliwa na Nani na kwanini? na baada ya ripoti hiyo kutolewa nini kitafuata?

Halafu kwanini ni Makonda tu na wala si Ma RC wengine?

Naomba mwenye majibu anisaidie
Agenda 2025
 
Hajavunja Sheria, ila hiyo michango ni ya nini anayoomba/kulazimisha

Lissu ana mamlaka ya kuweka watu ndani!?
Ahahahahaha! Kumbe kwakuwa hana mamlaka ya kuweka watu ndani ndio maana Lissu anachangiwa!? JF, The home of great thinkers! Ahahahahaha!!
 
Back
Top Bottom