Pre GE2025 Nani ameandaa kinachoitwa Ripoti ya Miezi 6 ya Makonda? Kwanini na ili iweje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kabla ya yote naomba kuwapa pole Wafanyabiashara wenzangu wa Kariakoo kwa kuangukiwa na jengo, nimeguswa moja kwa moja na ajali hii kwa sababu nina washirika wangu wa kibiashara wamepata janga, tumuombe Mungu awafanyie Wepesi, Amina.

Kwa kadri ya Umri nilio nao na kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kukumbuka kuona wala kusikia Mtumishi wa umma wa ngazi ya Chini kama RC akijifanyia ama akifanyiwa tathmini (ripoti) ya kipindi fulani cha uongozi wake (Niko Tayari kusahihishwa)

Sasa huko Arusha kuna jambo linaloendelea, kwamba eti Mtumishi wa Umma ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo ndugu Paulo Makonda anatoa ripoti ya Utumishi wake wa Umma kwa kipindi cha miezi 6 alichotumikia kazi hiyo!



Ripoti hiyo inatolewa ili iwe nini? kwanza imeandaliwa na Nani na kwanini? na baada ya ripoti hiyo kutolewa nini kitafuata?

Halafu kwanini ni Makonda tu na wala si Ma RC wengine?

Naomba mwenye majibu anisaidie
 
Huu ni muendelezo wa ushenzi wa awamu ya dikteta uchwara.

Mtu ataanzisha kikampeni uchwara chake akamue wafanyabiashara halafu wakimnyima awawekee zengwe, hiyo ripoti si akamsomee boss wake aliyemteua hizo PR stunts za nini?

Angalia hapa chini lile jambazi la Hai lilikuwa na kampeni eti ya kueleza mafanikio ya ilani ya CCM kwa miezi 6 ya uteuzi wake wafanyabiashara wanapitishiwa mchango ole wako ugome ndio wale waliokiona cha moto kwa kupewa kesi za uhujumu uchumi.

Sasa hili zero brain limekaa likaona hakuna anayeliongelea linaibuka na huu upumbavu.
 
Daaah
 
Hutaki uwazi? Wananchi kupata taarifa ya utendaji na utekelezaji ni nongwa?
 
Tayari ishu ya kutuhumiwa kujaribu kumuua Lissu imeshan'gang'ania anahangaika kujibu
 
Ni upuuzi mtupu, ndio maana eti muongozaji ni Zembwela ambaye kiukweli sio mtu mwenye taaluma yeyote ya uandishi, siasa au uchumi bali uchawa tuu.
Ila kwa majibu aliyotoa kuhusu Tundu Lissu ameingia cha kike
 
Maamae Sabaya huko aliko. Ametesa sana wafanyabiashara yule mbwa. Alistahili Risasi ya kichawa yule mbwa kichaa
 
Ya tundu lissu yamekushinda?!!! Kama huna mada tupia basi hata picha za watoto waliopo huko ulaya....yaani raia wa ulaya.
 
Wote hao wameshaona rais aliyepo ana uwezo mdogo hivyo wameamua kuanza kampeni mapema
 
kwa wasio na malengo na wasio na mipango mikakati hii itakua haina maana kwao..

But this gentleman, Paul Christian Makonda, Arusha RC, is a really visionary and modern leader of new era 🐒
 
Ukiendelea kfkria mamb ya Tanzania mwisho wasiku utakufa maskn ushndwe kuwachia kzaz chako njia ya kufanikiwa kwa urahis ss tufanye kaz kwa bdii tu
 
Kuna Sheria yoyote amevunja kwa kutoa hiyo ripoti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…