Nani amekosea hapa kati yangu na mzungu?

Joined
Nov 23, 2018
Posts
94
Reaction score
202
Salaam wanajamvi!
Wa baadu!
Wilaya ya Liwale, Lindi ni miongoni mwa wilaya zinazonufaika na huduma ya miaka mitatu ya Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF).

Liwale kwa sasa imekuwa Jamii mseto (multi-ethnic) kwani kupitia wafanya kazi wa MSF, tuna wazungu, wa Asia n.k

Nilikuwa nikisikia kwa baadhi ya wateja wa hospitali ya Wilaya kuwa wazungu mara kadhaa wamekuwa wakionesha dharau kwa wenyeji ila sikuamini.

Juzi nikiwa mapokezi ya Hospitali ya Wilaya, alikuja mzungu (mdada) akasimama karibu na nilipoketi, hakuna salamu na akanigeuzia mgongo. Wateja wenzangu pale mapokezi walimtazama kwa kumshangaa yule dada mzungu aliyeonekana kukosa uungwana.

Nikaona isiwe tabu kwani salamu shingap, wacha nimaalimie mimi. Mambo yakawa hivi:
Maalim: Habari gani ( huku nikimpungia mkono)
Mzungu:........ (kimyaaaa)
Maalim : Habari gani !
Mzungu: [Kwa ukali]...
If someone turns her back to you, it means she doesn't want to say hello....
Maalim: I'm very sorry madam.
Mzungu: .....[ akaondoka pale kwa hasira].


Sasa wadau naomba kujua ikiwa mimi ndio nimemkosea mzungu kwa kukiuka itifaki za salamu kama alivyonieleza au ni mzungu ndiye aliyenikosea?
 
ulitakiwa umtie kofi la takle alafu ulibinye, sidhani kama alikuwa anahitaji salamu, na ndio maana aliondoka Mkuu, next time mzungu akija bila salam akasimama mbele yako we mshike takle, binya kama unakamua mawese, visa na Safari huanzia hapo.
 
Utakua na "D" 2 wewe!
 
bAada ya kufika chuo na baadae dasilamu nilgundua sio lazima kila mtu usalimiane nae au uzungumze nae

Na kuna wakat unaweza kuwa karibu na kikundi cha watu wanapga story sio lazima uchangie story zao unaweza ukapga kimya tu,maana kuna wajinga wakiwa na mastory yao hata kama unayajua unaweza ukachangia na hata wasikusikilize hii tabia hasa kwa dasilamu
 
ulitakiwa umtie kofi la takle alafu ulibinye, sidhani kama alikuwa anahitaji salamu, na ndio maana aliondoka Mkuu, next time mzungu akija bila salam akasimama mbele yako we mshike takle, binya kama unakamua mawese, visa na Safari huanzia hapo.
😜🤣🤣🤣🤣 Mkuu una taaluma ya uwakili? Ili awamu nyingine nifanye km unavyonishauri, akinishtaki tu kwa udhalilushaji, wakili utumie maarifa yako kunitetea.
 
Fanya kilichokupeleka, mengine ni kujigonga gonga kwa watu wasiotaka kusumbuliwa
 
Kwahiyo alisimama na kukupa mgongo bila kusema shida yake iliyomleta hapo?

Kwa kawaida anayefika sehemu ndiye anawasalimia alio wakuta,so hapo aliyekosea ni wewe,
Hivi ingekua ni mbantu kafanya hivyo ungemsalimia? ungemnyamazia baada ya kukujibu vibaya?

Wazungu wanawadharau kwakuwashobokea,kitendo cha wewe kuanza kumsalimia ameshajiona yeye ni superior na wewe ni inferior kwake,

Siku nyingine acha shobo na kujipendekeza,itakujengea heshima kwenye jamii iliyokuzunguka.

Yangu ni hayo tu,
The rest it's up to you.
 
Nilikaa na jirani mzungu kwa miaka 8 hata siku moja hatujasalimiana
Wwmefundishwa tangu wadogo kutosalimia strangers
Sisi tunawalaghai watoto kwa kuwapa pipi na mwisho mnawapitia wakiwa wadogo
Wao kwa wao hapa kwao hawasalimiani kama hawajuani
Mtasalimiana kama kazini au umepeleka mzigo kwake na sio lazima pia
Kwa kifupi hawapendi kujuana
Tujifunze na ya kwao
Usijali wewe huna kosa na yeye ndivyo alivyofundishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…