Maalim Raphael
Member
- Nov 23, 2018
- 94
- 202
Salaam wanajamvi!
Wa baadu!
Wilaya ya Liwale, Lindi ni miongoni mwa wilaya zinazonufaika na huduma ya miaka mitatu ya Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF).
Liwale kwa sasa imekuwa Jamii mseto (multi-ethnic) kwani kupitia wafanya kazi wa MSF, tuna wazungu, wa Asia n.k
Nilikuwa nikisikia kwa baadhi ya wateja wa hospitali ya Wilaya kuwa wazungu mara kadhaa wamekuwa wakionesha dharau kwa wenyeji ila sikuamini.
Juzi nikiwa mapokezi ya Hospitali ya Wilaya, alikuja mzungu (mdada) akasimama karibu na nilipoketi, hakuna salamu na akanigeuzia mgongo. Wateja wenzangu pale mapokezi walimtazama kwa kumshangaa yule dada mzungu aliyeonekana kukosa uungwana.
Nikaona isiwe tabu kwani salamu shingap, wacha nimaalimie mimi. Mambo yakawa hivi:
Maalim: Habari gani ( huku nikimpungia mkono)
Mzungu:........ (kimyaaaa)
Maalim : Habari gani !
Mzungu: [Kwa ukali]...
If someone turns her back to you, it means she doesn't want to say hello....
Maalim: I'm very sorry madam.
Mzungu: .....[ akaondoka pale kwa hasira].
Sasa wadau naomba kujua ikiwa mimi ndio nimemkosea mzungu kwa kukiuka itifaki za salamu kama alivyonieleza au ni mzungu ndiye aliyenikosea?