Nani amelielewa tangazo hili la Bank of Tanzania (BoT), atufafanulie!

Nani amelielewa tangazo hili la Bank of Tanzania (BoT), atufafanulie!

Kwammba noti ya mwaka 1985 ambayo ilishatokewa tamko kama hili kwamba si halali tena, ghafla leo zinakuwa halali?! Au kuna mtu ana noti zake za zamani anataka kubadilisha ndio wanampa mwanya?
Swali gumu ila nadhani hawa wanaoununuaga pesa za zamani huko mtaani wana jibu. Maana unakuta mtu na kiti na meza yake kabisa ananunua noti za zamani
 
Kuna jambo kuuubwaaa pesa hakuna wana siasa wame ficha pesa mingi sanaaa ajili uchaguzi......zinatakiwa kurudi kwenye mzunguko....kazi kwetu watanzania wanasiasa wanasimamisha uchumi wa nchi sio wafanya biashara ? Only in Tanzania.....wafanya biashara ndio hao wana siasa....
 
Lengo wachapishe noti mpya yenye picha ya muuzaji hovyo wa maliasili zetu na kuacha za kwao.
 
Tangazo ni hili
--
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOA KWENYE MZUNGUKO NOTI ZA ZAMANI ZA SHILINGI YA TANZANΝΙΑ

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuhusu zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa. Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili, 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia katika kufanya malipo popote duniani; na benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Hivyo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani, kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.

Kwa taarifa/msaada zaidi tafadhali wasiliana na: Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939 Dar es Salaam; au kwa Barua Pepe: info@bot.go.tz au botcommunications@bot.go.tz; au kwa simu +255745 802 007.

Emmanuel M. Tutuba.

GAVANA

View attachment 3135997

Bot bana wanatoa tangazo bila hata picha. Sasa watoto wa Gen Z watajuaje not za 1985? Walete picha za pesa hizo.
😂😂
 
Kumbe ukifanya hivi ndo unaboresha Maisha ya wananchi wako, du acha nitoke 🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom