Salam wakuu,
Straight to the point, Stamina Shorobwenzi ametoa ngoma mpya inayoitwa Underrated ambapo humo amewashirikisha Motra The Future, Maarifa, Boshoo ze Son, Dizasta Vina ( The Black Maradona) na P Mawenge. Kwa ambao mmebahatika kuisikia, mnaonaje Nani ametisha humo ndani? Binafsi, Dizasta hajaniangusha
Stamina Ametuletea Jina la wimbo "Underrated" tuanze kwa kujua maana ya underrated ni nini ndio tutajua nani Ametisha humo
Kwa lugha rahisi kabisa Underrated ni mtu au kitu ambacho kiuhalisia kina uwezo mkubwa/umuhimu mkubwa/ufundi mkubwa/thamani kubwa/nguvu kubwa ila ni tofauti na vile jamii inakichukulia
Haya turudi kwenye Verses za wakali wetu tuangalie je ni Nani kaweza kubakia kwenye Mada ya wimbo? Kwangu Mimi list itakaa namna hii
1.Dizasta Vina
2.Mawenge
3.Stamina
Hao ndio walioelewa Assignment ya neno Underrated, ila kwa upande wa Boshoo,Maarifa na Motra wao ni either hawakuelewa theme ya wimbo au ni basi tu waliamua kuchagua mistari ambayo kwao waliona ni mikali
Udhaifu wa Boshoo ni mmoja, anapenda sana kwenda na mzuka wa Hadhira haijarishi atarap kuhusu nini na jamaa anarudia sana mistari, so inamfanya kuwa yuko too predictable, kuna mistari yake kamwe hawezi kuiacha
ukitaka kuthibitisha nenda mitaa ya dakika 10 za maangamizi kamskilize, alafu nenda kwenye Ngoma zake ukaskilize pia, utakuta mistari ya kwenye underrated kashaichana kule kitambo na vilikuwa havina uhusiano na wimbo wa stamina ila kapachika tu, Ngoma Kali kabisa ya Boshoo ni Nilipotoka ft Duke Tachez
Mwisho wa siku, hivi sasa tuna uhaba sana wa wasanii ambao wanaweza kustick kwenye Mada mwanzo mwisho, kama ilivokuwa kina Prof jay,Juma Nature,Afande sele,Jay Moe,Solo Thang,Daz Nunda,Fid Q, Langa,Ngwair nk
Kwa hivi sasa wasanii ambao wanauwezo wa kustick kwenye Mada mwanzo mwisho, wa Kwanza kabisa ni Dizasta, huyu kwenye hii case hakuna tena wa kumgusa maana anaweza kuandika kitabu kabisa achilia mbali kustick kwenye Ngoma ya dkk 10, huyu labda asimame na legend Prof jay
Akifuatiwa na Songa,Mawenge na Rapcha, hawa nao wako vizuri sana kwenye kubakia kwenye Mada au story telling, kama Mawenge ni Hatari sana huyu jamaa, pia Rapcha hayuko nyuma anajitahidi sana
NB, haya ni maoni yangu Tu.