Mkuu hapo kale mamlaka ndio zilikuwa zina control dini maana yake siasa ndio zilikuwa zinaamua kulinga na matakwa na hata machapisho yalitegema nani atatawalaNeno Injili ni neno lenye asili ya kiarabu ambalo shina lake linatokana na neno "euangelion" lenye asili ya kigiriki lenye kumaanisha "habari njema" ambalo liliingizwa kwenye lugha ya Kiarabu toka kwa wakristo wa Syria.
Na Torati ni neno linalotokana na neno la Kiyahudi "Torah" ambalo linahusisha vitabu vitano vya Sheria vya mussa vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania.
Lakini kumekuwa na shutuma kwamba Torati na Injili zilizopo Sasa zimechakachuliwa na siyo zile halisi za zama hizo.
Jee ni nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi ili tufanye ulinganisho tujue hizi Torati na Injili zilizopo sasa zilipunguzwa ama kuongezwa nini?
If the Qur’an says the Gospel came from Allah…
And if it says no one can change His words…
Then why do some say the Gospel was lost?
Truth doesn’t contradict itself. It confirms itself.
View attachment 3530865
Quran hii unayosoma Leo ni mchakato uliokamilika juzi tu hapo ukitaka nakutajia Hadi kamati yote kwa majina waliotengeneza standardization,ni 1924 hapo Misri Cairo Al Azhar University
Cha kuchekesha sasa ,Sio Saudia Arabia,Yemen, kufaa , Baghdad ambao Wana manuscript za Quran za karne ya 7 au 8 ,
Saudia Arabia nyumban kwa uislamu,iliwabidi Hadi 1985 ndipo waikubali hii Quran kutoka misri
Manuscripts za Quran zilizopo ni zile za Birmingham na sanaa , ambazo sio za karne ya 7a 8 ,sio za Uthman,
Na ni vipande vichache tu na zinatofautiana na Quran hii ya Leo ambayo wewe Umedanganywa ni ya toka miaka 1400 iliyopita
Unajua kwanini watafiti wanapigwa vita wakitaka kufanya research kwenye manuscript za Quran za Birmingham na sanaa?
Angalia biblia ,Ina Manuscript nyingi za kale ,
Leo ukienda pale Qumran measum hata uwe mufti unaruhusiwa kufanya research na kuona jinsi Maandiko ya agano la kale yalivyotunzwa kabla hata ya Yesu
Na wengi wanaowadanganyeni kuwa maandiko yaliharibiwa ,wamefika hapo wanaujua ukweli ,ndio maana huoni wakijibu hoja ,wamewaachia nyie hili bomu
Hizi picha hapo ni Qumran measum,mtafiti amefika anafanya research kuhusu Dead sea scrolls
Na kutokana teknolojia kuendelea imeonekana ni za mapema zaidi ya walivyodhani awali,
Hizi dead sea scrolls Zina Torati, zaburi ,vitabu vya manabii wote ikiwepo kitabu kizima cha isaya ,Yeremia ,n .k
Kuna kitabu cha Books of Giants walilikuta humo
Ni kitabu kimoja tu hawakukikuta cha Esta
Hapa sijagusia Septuaginta
View attachment 3530614View attachment 3530615View attachment 3530617
“Ni kweli Qur’an ya Cairo 1924 iliwekwa rasmi kwa madaris, lakini hii ni standardization ya uchapaji, si kuunda Qur’an mpya. Manuscripts za Birmingham, Sana’a na zingine zinaonyesha Qur’an ilikuwa ikisomwa kwa karne nyingi na tofauti ndogo za lafdhi tu, na haya hayaathiri mafundisho ya msingi. Tofauti ndogo kati ya manuscripts ni ya kawaida hata katika Biblia. Hii inathibitisha urithi wa maandiko wa dini, si kubadilishwa kwa kipindi cha karne chache zilizopita.”
Unajua kuwa Quran Haina hata manuscript moja tu ya karne ya 7 au 8
ili Hali biblia Ina Manuscript za kabla ya Yesu
Inakuwaje Quran ya juzi tu hapa INAKOSA angalau manuscript za Uthman
Wakati vitabu vya Aristotle vina manuscript
Kwanini Quran inasema mkaulize kwa waliopewa kitabu?
Je haikujua kuwa vimeharibiwa?
Halafu hiyo Yeremia 8:8 context yake sio hiyo unayosema
Kingine unawezaje kutoa ushahidi Kwenye kitabu unachodai kimeharibiwa ?
Hii inaonyesha kuwa maneno fulani ya asili yalibadilika au kutafsiriwa tofauti.
Paulo alikuwa muuaji mwanzoni, na baadae alibadilika na alishirikiana sana na wanafunzi WA Yesu kueneza injili
Hoja kwamba Paulo alikuwa kiongozi wa mauaji au alikuwa kinyume na wanafunzi wa Yesu ni si sahihi.
Biblia inathibitisha kwamba Paulo alikuwa mtumishi wa imani ya Yesu na aliwasaidia wanafunzi wengine kueneza Injili.
Kwa mfano, Waefeso 2:20 inasema:
20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
Paulo aliandika barua zake akishirikiana na Petro, Yohana, na wanafunzi wengine wa Yesu, si dhidi yao.
Aidha, Matendo 9:15-16 inafafanua kwamba Paulo aliteuliwa na Mungu kueneza injili kwa mataifa yote, si kuwaua wanafunzi wa Yesu. Wanafunzi walioshuhudia maisha ya Yesu waliendelea kushirikiana na Paulo, na hata wakubwa wa Kanisa walimkubali, ikionyesha wazi kwamba Paulo hakuwa kiongozi wa mauaji bali mtumishi wa kweli wa Injili.
Mkuu usiwapangie silaha za kutumia.Kutumia Chatgtp Kujibu maswali yanayohitaji tafakari ya kina siyo sahihi.
Kumbe hii ni vita?Mkuu usiwapangie silaha za kutumia.