Nani ana uchungu na elimu yetu?

Nani ana uchungu na elimu yetu?

Black Legend

Senior Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
174
Reaction score
301
Kupitia wizara zake za Wizara ya Elimu na TAMISEMI.....Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imeonesha nia na juhudi kubwa za kuwekeza katika ujenzi wa madarasa mapya na pia kuongeza shule mpya ikiwa ni pamoja na ukarabati wa majengo kwa shule kongwe zenye uchakavu.

Ongezeko la miundo mbinu hiyo imeendana sambamba pamoja na uwepo wa sera ya ELIMU BURE kutoka elimu ya awali mpaka sekondari, kwa jicho la kawaida ni jambo zuri na la kupongezwa....

Kwa mdau wa elimu, haya yote ni muendelezo wa miaka mingi wa serikali kujenga miundombinu na kuiboresha........kuanzia kipindi cha BENJAMINI WILIAM MKAPA, JAKAYA KIKWETE, P. MAGUFULI mpaka sasa DR. SAMIA SULUHU. Katika vipindi vyote hivi ujenzi katika sekta ya elimu umekuwa ukipewa uzito mkubwa.

Pamoja na uwekezaji mkubwa huu wa miundombinu (infrastructures) bado elimu yetu imekuwa ikishuka siku hadi siku. Kwa kurejea matokeo ya kidato cha pili yaliyotolewa wiki iliyopita , ripoti inaonesha kuna ongezeko kubwa la kufeli kwa wanafunzi. Moja ya sababu kubwa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa TAMISEMI ni UHABA WA WALIMU KATIKA SHULE ZETU.

Ni kwa muda mrefu sasa serikali imekuwa ikipigiwa kelele na wadau wa elimu kuwa kuna uhitaji mkubwa wa walimu katika shule zetu, lakini eneo hili limekuwa ni tatizo kubwa kwa serikali kulifanyia kazi.Matatizo mengine ni kama: MITAALA ISIYOKIDHI MAHITAJI YA JAMII YETU(Bado haijawa solved), SERA YA MATUMIZI YA LUGHA (Bado ni utata), MAZINGIRA DUNI YA KAZI KWA WALIMU, MASLAHI DUNI KWA WALIMU......nk.

Bado hakujawa na dhamira ya dhati ya kila kiongozi anaeingia madarakani kuiwekea elimu yetu kipaumbele kwa kuzitatua changamoto zilizobainishwa hapo juu na kuifanya elimu yetu kuwa ELIMU BORA na sio BORA ELIMU.
 
Back
Top Bottom