Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,435
- 1,995
Salamalleikhoom wakuu!
Nataka tujadili kuhusu mada au hoja hapa JUU!
Biashara zote za bidhaa zinatawaliwa na aina moja ama nyingine za vipimo ili kuhakikisha kwamba MTEJA anauziwa bidhaa husika kupitia kipimo ambacho mteja na mfanyabiashara wana uhakika nacho.
Kwamfano ukinunua nyama au mchele unapimiwa kwa mzani ,kilo kadhaa kwa shilingi kadhaa. Tena Kuna taasisi maalum inayosimamia vipimo iwe mizani au mita, Lita, mita nk. kwa biashara zote isipokuwa hii biashara ya bundles za simu!
Swali ni Je Mimi kama mteja, ninaponunua kifurushi cha airtime au MB za internet kwa shilingi kadhaa halafu hakuna namna ya KUHAKIKI kama ni kweli nimetumia MB au dakika nilizonunua bali ni mtandao tu mwenye kipimo; yeye anaona hicho kipimo huko aliko kama ni dakika 5 kweli au MB 1 au 2. hii ni haki?
Hawa TCRA na 'weights and measures' hawana MAMLAKA kwenye biashara ya huduma za simu? Kama ndiyo, kwanini?
Hakuna asiyejua kwamba biashara ya huduma za simu inaingiza fedha nyingi kwa saa, dakika hata kwa sekunde! Fedha ya mwananchi. Serikali nayo inakusanya fedha nyingi kwa saa kama tozo mbalimbali.
Lakini ajabu ni kwamba mteja anaewaingizia fedha nyingi namna hiyo ameachwa akipigwa bila mtetezi au refa ili kuona kwamba anatendewa kaki kama anaponunua bidhaa nyingineadukani, sokoni nk. anaona kwenye mzani kilo kadhaa au luku anaona amelipa nini na amepata unit ngapi. Na anaweza kuona kama matumizi yake ni sawa au anaibiwa.
NAWASILISHA