BIBLIA TAKATIFU INASEMA NINI JUU YA UCHAWI?
Biblia inakubali uchawi upo, tusome katika bibilia tupate udhibitisho. “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israel”(Hesabu 23:23)
“basi Balaam alipoona ya kuwa wabariki Israel, hakwenda, kama hapo kwanza, ili kutafuta uchawi, bali alielekeza uso wake jangwani. Balaam akainua macho yake akawaona Israel wamekaa kabila kabila, roho ya Mungu ikamjia.”(Hesabu 24:1,2)
Kuasi ni kama dhambi ya uchawi. “kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na unyago; kwa kuwa umelikataa neon la BWANA, yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”. (1 samweli 15:23)
“Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu mimi ndimi BWANA.”
(Lawi 19:28),
“msiwaendee wenye pepo wala wachawi; msiwafuate; ili kutiwa unajisi na wao; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu”(Lawi 19:31
“akampitisha mwanawe motoni, akatama bao, akafanya uganga, akashusha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.” (2 wafalme 21:6)