Nani anafaa kujaza pengo la Ndugai?

James Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,206
Reaction score
1,509
Nafikiri mpaka sasa Watanzania wengi watakuwa wamepata habari kuhusu tukio la spika wa bunge kujiuzuru. Swali litakalofuata ni, nani anafaa kuziba pengo lake?

Mimi binafsi nafikiri Mussa Azzan Zungu ni mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo ya spika wa bunge.

Sababu ya kwanza ni kwamba Mh. Zungu ana uzoefu mkubwa wa kuongoza vikao vya bunge. Binafsi nimeshawahi kumuona mara kadhaa akiongoza vikao vya kamati za bunge kwa ufanisi mkubwa.

Pili, ni mtu anayekubalika na kuheshimika kwenye chama chake tawala na vyama vya upinzani.

Na mwisho, huyu mzee ni mtu mwenye busara. Kiti cha spika wa bunge kinahitaji mtu mwenye busara, hususan ukizingatia bunge ni mhimili wa malumbano hali inayopelekea wakati mwingine wabunge kupandwa na jazba. Kwahiyo, anahitajika mtu kama yeye ili kuweza kutuliza mambo.

Unakaribishwa kutoa mawazo yako. Unafikiri nani mwingine anafaa kushika nafasi ya uspika?
 
Mtu yoyote ambaye hakishindwa kutetea mtazamo wake juu ya serikali awetayari kujiuzulu.
 
Umeongea ushuzi!
 
Ungese pro max
 
Spika atatoka nje ya bunge na mama ndo atampendekeza ,believe on me brother
 
Dah sema katiba inabana ila hiyo nafasi ilikuwa ima mzee wa ubwabwa aka wakili msomi, Hashim Rungwe Spunda ama Generali Ulimwengu.
 
Kwa bunge hili la kijani yeyote anafaa
 
Mtu mingi sana!




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…