Nani anafaa kuwa man of the match kwenye game ya leo kati ya Tanzania na Uganda?

Mara nyingi viungo wakabaji huwa hawapewi sifa zao kwakuwa huwa hawapigi chenga, kanzu wala kuweka madoido.

Lakini huwa wana kazi kubwa sana ya kukata mashambulizi dhidi ya timu pinzani. Na hapa ndipo ninapompa credit Erasto Nyoni. Leo ameweza kuwafanya Waganda wasipige zike pasi zao za haraka kuelekea langoni kwetu. Nyoni alikata kabisa mawasiliano ya Waganda.

Erasto Nyoni kwangu mimi ndio Man Of The Match! Nyoni leo amenikumbusha Luteni Jenerali Silas Mayunga "Mti Mkavu" jinsi alivyopambana na Waganda na utawala dhalimu wa Idd Amin Dada katika Vita Vya Kagera.
 
Kwa upande wangu ni John Bocco aliweza kucheza kwa ufanisi na aliweza ku assist almost magoli yote mawili ukiacha lile la penalt.
Usisahau Yule kiungo mkabaji WA znz
 
Reactions: Oii
Pamoja na yote tuwashukuru sana Cape Verde kwa kuwakazia Lesotho la sivyo hata tungeshinda kwa goli 100 tusingeenda popote! Kuhusu mechi ya leo mi naona timu nzima ilicheza vizuri! Aidha, viongozi wajifunze kuwa hamasa inaanza tangu mechi ya kwanza sio kusubiri mwishoni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna ubishi John Raphael Bocco leo kakiwasha yule mtu yaani nilikuwa sijui anacheza no ngapi.maana alikuwa anazunguka kote! Kukaba, assist mbili! 🔥 🔥 bila kusahau viungo wote hasa nyoni na mudhatir yahya nawapa tano
 
Hamna cha kuwashukuru. Wao pia walikuwa na nafasi wameshindwa. Ni juhudi za stars.
 
JOHN BOCCO... Kapteni wa Simba sc.
ametengeneza chance 2 za magoli.
 
Reactions: Tui
Kweli mkuu.. wanakuja mwishoni kama vikojozi bhana.
Yote kwa yote EAST AFRICA NI ZAMU YETU
BURUNDI
KENYA
UGANDA
TANZANIA.
 
Vp mkuu, kwa jinsi ulivyoangalia ile mechi,hakuna mchezaji wa Yanga alietoa mchango wake vizur uwanjan mana nakuona kiaina flan hiv
Nimekuchanganya na wasifu wa Bocco... no siko huko mkuu.
Yondani, Gadiel hata Fei toto wamepiga kazi nzuri ... Kazi ya Cotton nani hajaiona leo mkuu
Nitoe huko mkuu mi sio wa hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…