Nani anafaidi utajiri huu wa Tanzania?

Tanzania ni masikini kwa sababu ya UBINAFSI wa viongozi wetu wa ngazi za juu serikalini .

Reginald mengi ni tajiri mkubwa ni kiongozi wa serikali?
Bakhresa ni tajiri mkubwa mno ni kiongozi wa serikali?
Umaskini wa nchi wa kujitakia.Ukiwa mvivu wa kutumia fursa zilizopo eneo lako usitafute mchawi.
 
Kuna viongozi wachache wameilaanisha ardhi ya Tz
 
migodi ya dhahabu mingine imefungwa na mingne dhahabu ndio inaisha lkn bado hatujanufaika na hizo dhahabu.
 
This things got complicated...ngoja niendelee na kilimo changu cha miti na migomba
 
Ahsante kwa taarifa mkuu, ila kimoja kikubwa ulichosahau ni kwamba tanzania ina CCM iliyoikalia hii nchi kwa zaid ya miaka 50 bila lolote zaidi ya maneno mengi.
 
Mleta uzi huu, nakupongeza sana na aliye juu Mungu, akuzidishie hekima uliyonayo, sema Aamiiin!

Nimejikuta nikighadhabika baada tu ya kumaliza kusoma utajiri wa nchi hii, najiuliza mambo mengi mengi tu na kujijibu mwenyewe.

Na katika hali ya kawaida, bado kuna utajiri mwengine haujaufikia na upo naamini, ila kwa sababu raia sisi sio watu wa kufuatilia, wajanja wanapiga tu pesa kimya kimya.

Najiuliza, wale vijana wasio na kazi kipindi cha kampeni wanavalishwa nguo za rangi na kukesha juani masaa mengi, na wengine kutukana wenzao wa upande wa pili mitandaoni, tena kwa posho ndogo tu na wengine wanajiita wasomi, wanayajua haya? Wanafahamu wanayemnadi atafaidika vipi?! Najikuta nikisikitika tu!

Ahsante!
 
Wanasiasa kiukweli, wametufikisha hapa, nakumbuka ile misemo yao mingi mingi tu ya miaka ya nyuma, mfano VIJANA NI TAIFA LA KESHO, bila kutoa ufafanuzi wa ziada, ni kiaje awe Taifa la kesho? Ila miaka ya hivi karibuni wamebadili (si unajua kubembeleza kula), eti VIJANA NI TAIFA LA LEO, na bado hawafafanui.

Wanatoa mikopo vyuoni, japo wapo wanaoikosa, ila ukimaliza tu chuo na kuomba kazi, wanataka UZOEFU USIOZIDI MIAKA MITANO, hapo lazima ukose sifa na awekwe wa mlengo wao ili mrija uendelee kunyonywa.

Wa-Tanzania, tumekuwa (japo siyo wote), watu wa matukio sana, yaani utakuta wasomi wapo wapo tu, hawawi wabunifu, ila ni kila baada ya kazi, nani kasema nini na wapi, ndiyo habari hizo, mfano Raisi katangaza mshahara wake (inasemekana), yaani wengi wanam-support bila kujua hayo aloyoyataja mleta uzi atafaidika vipi nayo huyo kiongozi.

Tu wepesi sana kulaumu, kuliko kufanyia kazi yale yaliyo maovu. Tu wepesi pia kuwaamini wanasiasa bila kufikiri kwa msaada wa jicho la tatu.

Ahsante!
 
Hapa muchawi ni nani???????????????????????????
Aise mimi nataka kulia
 
Ahsante kwa taarifa mkuu, ila kimoja kikubwa ulichosahau ni kwamba tanzania ina CCM iliyoikalia hii nchi kwa zaid ya miaka 50 bila lolote zaidi ya maneno mengi.


tatizo wale viherehere wa kuuliza na kuibua hoja zenye vithibitisho....
wengne ukutwa na mauti au kutolewa kucha na meno....
 
Ila nashauri njia pekee ya kujikwamua na ugumu huu wa maisha, ni kuanza kuzijenga akili zetu katika kujiajiri kibiashara, japo pia vikwazo vitakuwepo sana tu (Rejea wimbo wa Remmy Ongala - Marehemu-, uitwao Mama), utajisikia kama siyo kulia basi ni kuhuzunika.

Tuwaache wanasiasa wafanye siasa, japo tuwasimamie kwa utendaji wao na siyo kushabikia kila wanalosema, yaani watu inafikia hatua tunazisizisha akili zetu kisa tu mwanasiasa fulani mpendwa kasema nini na wapi, upande wa pili wa alichokisema hatujisumbua kuhoji bongo zetu kutupa tafsiri.

Nashukuru, binafsi sina ushabiki wa kisiasa hadi kuvaa sare zao, bali nina ushabiki wa maendeleo niyaonayo ya nchi, yaani upinzani ama ushabiki wangu upo kwenye damu na siyo nguo na kutusi wengine.

Naomba niishie hapa, nahisi ghadhabu kidogo imenishuka. Tufanye biashara zetu kihalali, kazi za halali, wanasiasa wasituchanganye.

Ahsante!
 
Mkuu wa tz sisi hasa vijana ndo tatizo tukipewa buku mbili tunaanza kushikana miguu
 
KWA NINI TUNASHINDWA KUTUMIA HUU UTAJIRI?

Mkuu hii mada yako nimewapa wanachuo waijadili hili ndio jibu wametoa.
Mmoja anasema jina la mleta maana ni la kihehe ambalo ni la pale Iringa.Akasema iringa ya wahehe ina fursa nyingi mno lakini wahehe ni maskini wa kutupwa.Matajiri wakubwa wa Iringa ya wahehe ni wafuatao ambao waliona kuna fursa Iringa ya Wahehe wakaona wazitumie.Matajiri wa Iringa ya wahehe ni wafuatao
1.Waarabu akina ASAS &CO
2.Wakinga
3.wachaga
4.wabena
Hata mashamba makubwa ya miti yanamilikiwa na watu toka mikoa mingine.

Akasema wahehe ni wavivu kutumia fursa zilizopo mkoani kwao.

Mleta maada labda utueleze tu huo utajiri na raslimali za huko kwenu kwa nini hamtaki kuzitumia hadi uje kuuliza nani anafaidi humu jamii forums ilitakiwa ufanye utafiti kwenu kwanza.
 
Mkuu wa tz sisi hasa vijana ndo tatizo tukipewa buku mbili tunaanza kushikana miguu


tatizo sio chama wala siasa, tatizo ni wale watawala au viongozi wanaopewa dhamana na wananchi lkn wao wanageuka kuwa mawakala wa wawekezaji nakusahau uzalendo.
 
Reginald mengi ni tajiri mkubwa ni kiongozi wa serikali?
Bakhresa ni tajiri mkubwa mno ni kiongozi wa serikali?
Umaskini wa nchi wa kujitakia.Ukiwa mvivu wa kutumia fursa zilizopo eneo lako usitafute mchawi.
Soma posts vizuri na kuzielewa kabla ya kutokwa povu, hapa.
Hao uliowataja wameingiaje kwenye uzi huu?
Kuna fursa gani Nyamongo kwa wazawa wakati watu wanaangamia kwa maji yenye sumu toka migodini?
Wengine wameuawa kwa kusingiziwa kuwa ni wezi.
Viongozi wanakwenda kuongea na wawekezaji badala ya wananchi, halafu kimyaaaa
Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini ingawa ina utajiri wote huo ulioko mikononi mwa wageni.
 
Mkuu nimesoma uzi wako hadi chozi limenitoka.nafikir vigogo wa awamu ya tatu na nne na familia zao.
 
mimi sitailaumu serikali pekee katika hili, bali pia watanzania wengi ni wavivu, hawapendi kujifunza na kujituma, ni watu wa kulalamika kila mara japokua pia serikali inazo lawama, pia sisi hatujaweza kufanya part yetu kama wananchi wazalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…