Nani anafaidika na ndoa?

Nani anafaidika na ndoa?

Huyo mke na watoto wote wapumbavu. Mke ataachaje nyumba yake kwenda kuishi kwa watoto as if mume kafariki? Na watoto watakubali vipi kuishi na mama yao na kumtelekeza baba yao?

Ifahamike siyo wanaume wengi wanakumbwa na masahibu hayo kwa hiyo yaliyomkuta huyo bwana ni ajali kama ajali zingine!
Wanaume wengi wanaishia hivyo...Zinatofautiana tu namna, ila kiujumla wanawake ndio wanafaidika zaidi...na wanajua hilo, ndiomaana wanajazans kwa mwamposa kuomba waolewe
 
Mwanaume huyu ana umri wa miaka 68. Ni mstaafu aliyefanya kazi maisha yake yote kulea watoto wake.

Alijinyima raha za dunia ili aweze kuwalipia karo ya shule (kwenye shule za gharama) na gharama nyingine za maisha kwa watoto wake nje ya nchi.

Sasa watoto wako vizuri huko Uropa na Amerika. Mkewe mwenye miaka 60 amemwacha mzee huyu na kuwafuata watoto wake kwenda kuishi nao.

Sasa mzee yuko peke yake nchini Kenya. Watoto wake wala hawamtafuti. Na sasa inabidi aanze maisha mapya kama kapera.

Anapambana na shinikizo la damu na magonjwa mengine ya uzee. Je, angeishi peke yake hadi lini?

Huu ndiyo ukweli kwa wanaume wengi wa tabaka la wafanyakazi wenye mke mmoja. Uzee wao kwa kawaida ni wapweke na katika hali nyingi, huzuni.

Jitahidi kadri uwezavyo, lakini wanawake wanapenda watoto wao zaidi ya waume zao, haijalishi mwanaume ni mtanashati kiasi gani. Kadiri anavyozidi kuwa mzee, ndivyo mvuto unavyopungua kwa mkewe.

Niambie basi, wanaume wanafaidika nini na ndoa?

Wanajinyima sana lakini wanapata kutambuliwa kidogo sana kwa kazi ngumu. Mwanamke huvuna faida zote kwani watoto mara nyingi huwa karibu na kumpenda zaidi anapozeeka...

Tuendelee kuimba "Nani kama Mama"...View attachment 2683800
Huyu kuna mahali alikosea wakati wa ujana wake.Mbaya zaidi wanawake ni watu wa vinyongo na visasi.mwanaume anapomtendea mke ndivyo sivyo yeye anasahau lakini mke anaweka moyoni.Matokeo yake ndiyo hayo.
 
Back
Top Bottom