Nani anafanya biashara ya Chipsi

strategist22

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
655
Reaction score
599
Yeah nataka nianze hii Biashara vifaa vyote tayari ninavyo bado sijapata sehemu natafuta maeneo ya Mbagala rangi tatu, kwa azizi Ally na tandika.

Nahitaji mtu anayefanya hii Biashara anipe mbinu za kufanya na za kuepuka. Ikiwezekana niende kwenye ofisi yake kupata uzoefu Kidogo.

Karibuni kwa ushauri, maelekezo, mapendekezo nk.
 
Wewe ulishawahi kufanya kazi kwenye biashara ya kuuza chips?
Unaijua hiyo biashara jinsi ilivyo?
Nini kilikusukuma kutaka kufanya hiyo biashara?

Kwanini ununue vifaa vya hiyo biashara kabla ya kudadisi namna hiyo biashara inavyofanyika.
Hello, ndio nimewahi kufanya kazi ila ni mkoani, changamoto haziwezi kuwa sawa kabisa na huko.

Kilichonisukuma ni hamu ya kupata kipato na kwanini Chipsi? Pesa ya kuanzia niliyonayo inatosha kwa Biashara hii sababu vifaa tayari vipo (kuna brother alifunga Biashara zamani) Ujuzi na uzoefu kiasi upo.
 
Inshort Biashara Kichaa hiyo. Gharama Za Mafuta / Gas / Umeme / Vijana wa Kazi / Rent

Ni Daily then uanze kuhesabu faida yako hapo nafuu ufungue jiko la Kitimoto cz pay / prepare as per order basis. Kuna Challenge Zake Ila Sio Kama Kwenye Chips.
 
Inshort Biashara Kichaa hiyo. Gharama Sa Mafuta / Gas / Umeme / Vijana wa Kazi / Rent

Ni Daily then uanze kuhesabu faida yako hapo nafuu ufungue jiko la Kitimoto cz pay / prepare as per order basis. Kuna Challenge Zake Ila Sio Kama Kwenye Chips.
Hiyo inategemea na location.

Ukipata maeneo mchangamko hizo hasara huoni kwani mauzo ni mengi.

Na sio kwa biashara ya chips pekee bali ni biashara yoyote kama mauzo ni makubwa hata kama faida ni sh mia tano kwa siku ukiuza mara mia tano si sawa na anayeuza mara kumi au kumi na tano tu.
 

Sawa Fanya.

Unapolala Wenzio Tumeamkia Hapo.

Sijui Lakini, Acha Ajaribu.
 
Inshort Biashara Kichaa hiyo. Gharama Za Mafuta / Gas / Umeme / Vijana wa Kazi / Rent

Ni Daily then uanze kuhesabu faida yako hapo nafuu ufungue jiko la Kitimoto cz pay / prepare as per order basis. Kuna Challenge Zake Ila Sio Kama Kwenye Chips.
Unafanya Biashara ya kitimoto ,Naomba ABC Kidogo.
 
Asante. Mkuu
 
Mkuu from my experience nilishakuwa na biashara za chipsi tatu, ni changamoto na mpera mpera plus kuroga ili kuvuta wateja,ila cha msingi sio shemu inayowaka tu ndio kuna wateja ila hata sehemu za nje ya mji unaweza fanya biashara vizur tu na ukapiga hela kimya kimya........

Tafuta sehemu watu wanapo hamia ambapo hakuja changamka sana ambapo unaweza fanya biashara bila presha, make sure unazoeana na boda boda wote wa mtaa huo then fungua goli la chipsi kwa mtaji mdogo tu ukiwa tayar na kabati lako na kisehemu chako, wala usiwe na mbwembwe nyingi uza chipsi tu na mishikaki nusu na mayai yako trey moja, hela ya kula uwezi kosa.

Kuna kijana wakati nipo vizur kidogo mwaka jana tu alinifuata akaniambia brother sina mishe mtaani ila nina experience ya kuuza chipsi nifungulie goli nikimbize, sikuwa na hiyana nikatenegeneza kibanda kiligharimu kama laki moja tu ,tukavuta umeme na kumuambia kazi kwako,ila akakaa kama miezi kadhaa hafungui kumbe alikula hela ya kununua vitu vidogo vidogo kama karai ,sahani,vijiko,

Kaenda kupiga mishe za tofali then akanifuata tena brother nimerudi nipo tayar kwa kazi ,ila sina kabati nikamwambia pambana upate kabati ntakununulia viazi na mafuta uanze kazi, kaongea na baba yake kammtengenezea kabati,akanicheki tena brother tayar kila kila kitu nikampa elfu 50 tu ya kuanzia ,ila huwezi amini dogo anapambana sana viazi anawajazia kinoma mpaka nikawa nashangaa nikamwambia aiseee usije ukaniambia mtaji umekata hiyo ofisi ni yako sitaki hata kumi unipe, akasema brother huku uswazi nawajazia hawa ili wakawaambie wenzao mwisho wa siku wateja wajae hapa........


Kumbe ndio ilikuwa uchawi ule aiseeeee, sasa hivi wateja wanakuja pale wanapanga folen ya kawaida na anauza ndoo kumbwa mbili hadi tatu.

Jamaa anauza hadi 80,000 per day......analaza 30 per day..........

Alafu yupo normal tu .hiij ishu kanichana jana baada ya kukutana nae .akasema brother nakushukuru sana nlikuwa nikiamka sijui pakwenda ila sasa mambo yanaanza kufunguka,nikashangaa sana yan ambae nlimfungulia kimasihara siingizi hiyo hela kwa siku ila yeye ana force anaingiza,lakin mdio maisha siwez kumuonea wivu kisa anapata kuliko mimi,

Chipsi inalipa wazeee ukipata sehemu poa isiyo na mambo mengi
 
Noted. Asante brother, nimepata mwanga, ila wewe umewai kuroga[emoji3]
 
biashara yenye mtaji kidogo lakini faida yake ni kubwa sana!!kama utakuwa makini kwenye matumizi.
 
Noted. Asante brother, nimepata mwanga, ila wewe umewai kuroga[emoji3]
Sijawai kuroga aiseee! Ila wa pembeni yangu anafanya mambo hayo anaweza akafunga siku mbili akirudi siku ya tatu amsha yake sio ya kitoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…