Nani anaifahamu Bwawani secondary School Morogoro?

mama yuva

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2010
Posts
226
Reaction score
47
Wapendwa wana jamvi,

Naomba msaada kwa yeyote anayeifahamu Bwawani sekondari, mazingira yake ya Bweni, upatikanaji wa maji, sheria za shule. Najua matokeo yake ni average, lakini mengine sifahamu. Tabia za wanafunzi kwa ujumla. Hasa hasa wa kiume. Kuna yeyote aliyesoma hapo ?
 
mama yuva mimi nimefundisha hapo kwanza shule inamilikiwa na jeshi la magereza tanzania, shule ina maktaba iliyosheheni vitabu na maabara zipo.

-chakula chao ni kizuri sababu shule inazingatia balance diet

-mazingira yake ya bweni ni mazuri tu

-maji yanapatikana bila shida yoyote sababu shule ina matank ya maji yakutosha

-sheria za shule zipo zinafanya kazi kwa mwanafunzi atakae zikiuka.

-tabia za wanafunzi ni nzuri sababu shule ni ya jeshi hivyo wanapewa malezi mazuri tu

Unaweza uliza chochote nikakusaidia ukiwa na tatizo.
 
Asante sana mambaenock. Umenipa moyo.

Barikiwa sana.
 

vipi mamba shule hiyo ni high school? ada ni kiasi gani you can contact me in 0784142757
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…