NANI ANAIJUA KESHO ?

NANI ANAIJUA KESHO ?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
NANI ANAIJUA KESHO??

MIAKA ya 1980's Mike Tyson alikuwa kwenye ubora wake kweli kweli usingemsogelea ulingoni wala kifedha nje ya ulingo.

MIAKA 8 mbele akamuajiri Donald Trump kama mshauri wake mkuu alikuwa ni Mike Tyson tena kwenye ubora wake.

HIVI leo mimi na wewe tunazungumza hapa Donald Trump ni Rais wa Marekani, Donald Trump si yule mshauri wa Mike Tyson tena , Mike Tyson huyu alieshuka kiuchumi mpaka kuwahi kwenda jela kwa kuhusishwa na cocaine.

MWAKA wa 2003&04
Fernando Jose Torres Sanz alichaguliwa kuwa Captain wa Atletico Madrid akiwa na umri miaka19 tu!! ,ndani ya kikosi hicho alikuwepo pia Diego Pablo Simeone aliyekuwa amemzidi Torres miaka 14 kiumri!!

NDANI ya uwanja Torres akawa Boss wa Simeone, Simeone akawa anapokea maelekezo ya Torres.

MWAKA wa 2015
Diego Simeone akiwa kocha wa Atletico Madrid alimpokea tena Torres kama mchezaji wake na si Captain wake tena.

NDANI ya uwanja Torres akawa anapokea maelekezo ya Simeone, Simeone akawa Boss wa Torres.

''MAISHA ni kama sarafu iliyorushwa juu hakuna mwenye uhakika ni upande upi itaangukia''
''HAKUNA anayekaa juu siku zote ni suala la muda na nyakati tu'', ''Boss anaweza kuwa kijakazi na kijakazi anaweza kuwa Boss kesho''
 
Back
Top Bottom