Kuingizxa majina mengi ili uonekane una point ni mufilisi wa mawazo na kuishusha heshima ya forum, Mtandao wangekuwa na hiyo nguvu basi wangechukua madaraka ya kina makamba, mwanri, na wote waliochaguliwa karibuni na muungwana mwenyewe, en angekuwa katibu wa ccm kama alivyokuwa akilalia macho,
jm ni mwanasiasa mkomavu aliyegombea urais mara mbili akashindwa, na hakuleta makelele wala kilio maana anajua kuwa siasa ni mchezo wa aina gani, na anajua kuwa kushindwa urais sio mwisho wa maisha kama wenzetu mnaotumia majina mengi mnavyotuambia, sasa ningependa kuwauliza kuwa baada ya Freeman kushindwa urais anatakiwa afanye nini aache siasa, au ajitayarishe kugombea tena?
Mzee MMJ, tunaelewa kuwa nia na madhumuni ilikuwa kubadili topic ili ile ya Zeee ipotee, goood works ila sio wote wajinga hapa, kuhusu jm ninasema kuwa ccm bado tunamuhitaji na ni majuzi tu ameendelea na ile kali yake huko tunduru ya kuisambaratisha upinzani, ccm 62%, chadema 3%, kelele za mlango hazimzuiiii kiongozi yoyote wa taifa letu kukosa usingizi, kuanzia ccm wala upinzani, Mwalimu na maneno yake yote amemuacha the man anaendela tena bado mpaka leo, na inavyoelekea ni mpaka ccm wenyewe tutakapo mwambia kuwa imetosha, na wanachi wa jimbo lake watakapo sema basi, otherwise tutaendelea kulia lia tu malecela! malecela! malecela! ccm inaendelea tu kutawala, wabongo maneno mengi ukweli hatuna wala matendo! ndio maana jamaa wataendelea kutuzia busara zao kwa shillingi millioni 100, sisi tunalia malecela!!!!! tuuuuuu!
mimi sielewi kiongozi asiyekuwa na influence anapokuwa ndiye kichwa cha habari hapa forum kila kukicha, hebu waombe maderators uone humu forum kuna ishu ngapi zinazozungumzia malecela na viongozi wengine wa taifa, au hata wa vyama vya upinzani, utashangaa mwenyewe maana ni karibu 50 against 0, lakini tunaambiwa the man sio influencial, in the last six months mzee amekuwa huko majuu karibu mara 10, between Swiss, London, na NY, hebu tuambieni kama that is the case na wastaafu wengine, maana hizi safari anazifanya kama mstaafu, na sio kama Veep wa ccm,
Ninarudia maneno niliyowahi kuyasema huko nyuma kuwa kwa mwendo huu wa wananchi na haya mawazo ninayoyaona hapa, cccm itaendelea kutawala daima kama sio milele, unajua enzi za utumwa masters walikuwa na tabia ya kuwafungia watumwa ndani ya nyumba wakati wa usiku na kuwaambia wasitoke nje, na wao masters walikuwa wakikaaa madirishani kuwasikiliza wakiongea, to their suprise watumwa walikuwa wakiongelea na kubishana sana kuwa nani kati ya masters wao ana hela zaidi ya masters wengine, na mke yupi wa masters wao aliyekuwa mzuri kuliko wake wa masters wengine, hawa watumwa hata siku walipoachiwa walikataa kabisaaa kuondoka wakidai kuwa watakufa bure na njaaa wakitoka utumwani pale!
Here we are, masikini wananchi wa bongo, Mungu aibariki tu nchi yetu! Maana kama ni kutegemea wananchi waje waigeuze nchi yetu, wananchi wenyewe ndio sisi!
kama mzee Jasusi ulivyosema "what a country"