Nani anajua sehemu nzuri ya kujificha

Nani anajua sehemu nzuri ya kujificha

bioto

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
1,261
Reaction score
2,097
Rafiki yangu alikuwa amesinzia tukiwa darasani, nikachukua simu yake nikabadilisha alivyosave namba yangu nikasave "lovely dad" (ndivyo alivyokuwa amesave jina la baba yake mzazi)
Nikamumia SMS "mwanangu nimeshinda millioni 100 toka BIKO, na sasa hivi tutakuwa na maisha mazuri. Acha shule njoo tupange tutafanya biashara gani"
Rafiki yangu baada ya kusoma sms akanyanyuka na kukusanya kila kilicho chake akaanza kuondoka.
Alipofika mlangoni mwalimu akamuuliza unaenda wapi bila kuomba ruhusa?
Akageuka akamwonyesha mwalimu kidole cha kati, akaachia mfyonzo mkali kisha akasepa.
Sasa hivi ananisaka kinyama, nani anajua sehemu nzuri ya kujifichia jamani.....!
 
Back
Top Bottom