Nani anakumbuka chupi za VIP?

vp jamani na yale mafuta ya mamisi ukijipaka unafuatwa na nzi hadi unalia maana unawafukuza hadi unachoka du! Jamani nyie acheni tu!
 
Umenikumbusha mafuta ya kujipaka ya ashant na sabuni ya Titani.Daa ni kitambo sana 1988.
 
Wakuu nakumbuka kaka yangu mmoja, alikuwa mitungi sana alipo amka akavaakanzu bila pensi basi dah ilikuwa aibu sana maana ndani alivaa V.I.P ambayo kila mtu aliona mistari ile ya rangirangi bila kificho. Yaani ilikuwa aibu maana tulikutana naye sokoni.
 
Mnakumbuka vita ya watoto wa uswahilini na magorofani, Pia watoto wa manzese na mbwa wao wolivyokuwa wanakwenda kula ukoko mlimani
 
 
Du hii kali sana,sasa hapo ticha alipogundua chupi iko kifuani action ya kwanza aliyofanya ni nini kabla ya kutimka
 
Hiyo ya kioo naikumbuka kuna jamaa alikuaga primary anaifanya hiyo sana,siku moja wanawake walimgundua wakaenda kumripoti kwa mwalimu mkuu,alanyukwa viboko huyo na suspension akapewa.Kuna jamaa mwingine huyo ndio alitoa kali alikua anamfuata msichana anamwomba shilingi ya kununua mandazi,mara nyingi wasichana wanamwambia hatuna,akiambiwa hivyo anamkomalia huyo msichana anamwambia unayo,halafu anamwambia kama hauna lete nicheki mfukoni akiruhusiwa kosa anaingiza huo mkono mfukoni anajifanya kupekecha kutafuta hiyo hela kumbe anagusagusa hiyo nanihii,akitoka hapo anafurahia anakuja kutuadisia,huyu jamaa sasa hivi ni engineer bosi mkubwa tu huwezi amini kuwa utotoni alikuwa mpumbavu kiasi hicho
 
Wandugu,
Miaka ile Mwl Nyerere alivyong'atuka katika Uongozi na kumpatia kijiti Mzee Mwinyi ndio tulianza kuvaa hizi chupi za kiume aina ya VIP.

Leo humu JF walioishi kwa kuvaa hizi chupi na mpaka zinapotea sokoni hawazidi hata 30%. Kuna kitu sitakisahau kwenye hizi Chupi;

Kwanza kwenye kufua - Ilikuwa rahisi sana kukauka na ilikuwa inakubali povu la sabuni ile mbayaa. Hata kama ulikuwa na hii hii moja tu yaaani ukiifua Usiku wa saa 2 mpakaa saa 1 asubuhi inakuwa imeshakauka kwa zile sehemu zisizo na baridi kali

Pili kwenye matumizi yake mwilini. Ilikuwa kama unacheza mpira basi ujiandae muda wowoote ngoma itakuadhiri kwenye kadamnasi.

Story kidogo;

Kwenye maunganisho yake chini kabisa kwenye miguu haikuwa imara. Siku moja jamaa alikuwa kwenye mechi kali sanaa, Tulikuwa tunashindania miwa na kiroba cha maembe, Sasa wakati mechi inaendelea fowadi wetu kumbe alikaatikiwa na chupi yake ya VIP kwenye maungio huku chini bila kujua nadhani ni katika zile purukushani za mpira, Wakati anakuja kuurusha mpira uliotaka huku nje ndio tukashangaa kiuno kimejaa rangi tofauti tofauti kama vile kavaa shanga kumbe banaaa Chupi ya VIP imekatika na imepanda juu yenyewe bila jamaa kujua, Tulicheka sanaa. VIP ilikuwa so funny !
 

Attachments

  • 1408677648620.jpg
    9.4 KB · Views: 739
Aisee umemikumbusha mbali sana, nimecheka sana.
 
Umenikumbusha mbali nakumbuka niliwaona watoto wa shule ya msingi wakiwa shuleni walikuwa kila mtu anavua kuonyesha mwenzake kama amevaa VIP. Ila mimi bisafsi sikuipenda hiyo chupi kwa sababu ilikuwa na tabia ya kumbana sana Mheshimiwa wangu kwenye suruali. jaman ilikuwa inambana mheshimiwa, kila wakati anakaa ametuna mpaka hata hewa hapati!!!!
 
Duh umenikumbusha mbali!Nakumbuka siku moja nimeivaa kwenye mechi,baada ya mapumziko navua tshirt ili nipunge hewa,nikaikuta makwapani!!!!

Duh ilikuwa aibu ya mwaka!Mashori kibao walikuwa uwanjani!
 
Duh umenikumbusha mbali!Nakumbuka siku moja nimeivaa kwenye mechi,baada ya mapumziko navua tshirt ili nipunge hewa,nikaikuta makwapani!!!!

Duh ilikuwa aibu ya mwaka!Mashori kibao walikuwa uwanjani!

hahahahahahaha
 
Dah e bwanae, nilikuuwa mdogo sana enzi hizo naishi hukooo kijijini, basi mzee akasafiri Kuna town akawanunulia kaka zangu wakubwa kila mmoja km zawadi. Wao kwa ushamba wao wakadhani ni bukta wakawa wanapiga nazo tizi uwanjani. Tumetoka mbali waungwana
 
Noma sana ilikua ni kama vile umevaa mwamvuli kwenye upepo maana usipokua makini upepo utakuadhiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…