Nani anakuwa desperate zaidi kati ya mwanamke au mwanaume?

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,100
Jamani eeh hivi inapofikia umri fulani ambao inaonekana sasa mwanamke au mwanaume anatakiwa kuwa kwenye ndoa na bahati mbaya anakuwa bado hajaona mwelekeo, nani anakuwa desperate zaidi kuingia kwenye ndoa, mwanamke au mwanaume?
 
Yeyote yule...
Ndio maana wengi tu wanaingia ilimradi.
 
Ni wanawake,ndio maana wakatengenezewa muv yao ambayo inaitwa desperate housewives....
 
Kweli we wa kitaa...ila usiharibu thread ya jamaa bwana ndo kwanza imeanza.Subiri mida mida alafu uniambie huko double D ni wapi!!

Aaah Lizzy Licious acha hizo bana.....ntakucheki kwenye skype mida mida basi au vipi?
 
Ni wanawake kwa sababu hawawezi kutafuta mme mpaka watafutwe!!!! Mwanaume uamuzi wa kuoa na kutooa ni wake. Mwanamke hata ukitaka kuolewa ni mpaka umpate huyo muoaji anayetaka kukuoa wewe.
 
Ni wanawake kwa sababu hawawezi kutafuta mme mpaka watafutwe!!!! Mwanaume uamuzi wa kuoa na kutooa ni wake. Mwanamke hata ukitaka kuolewa ni mpaka umpate huyo muoaji anayetaka kukuoa wewe.
Anhaa sasa kama ikifikia hali hii na bado hajitokezi mtu what happens au wanafanya nini?
 
Si ndo wanakuwa desperate
Sasa si ndio hapo kama mtu akifikia hapo hatua gani anaweza kuchukua? Atafute kwa nguvu au aweke tangazo gazetini kwenye front page au?
 
Kwa mtu kama huyo cha kufanya ni kuendelea kuwa desperate with time anaweza patikana "bora mume" si mume bora. Si unajua tena tabia za desperate? Kama kuwa king'ang'anizi; vyote vina work iko siku anapatikana walau wa kutolea nuksi.

Sasa si ndio hapo kama mtu akifikia hapo hatua gani anaweza kuchukua? Atafute kwa nguvu au aweke tangazo gazetini kwenye front page au?
 
Afu unajua nini BB; hata huko kwa wadhungu ambako mwanamke kutongoza si kitu cha ajabu; when it comes to proposing for marriage ni mwanaume ndiye anayepropose. Kwa hiyo ndio maana inabaki pale pale wanawake tunasubili kuombwa kuolewa hatuwezi kupiga magoti and say "will you marry me?" hhiyo haipo hata uwe umedata kiasi gani.

Afu unakuta msichana anachekelea jamaa ka propose; meaning alikuwa anataka kuolewa na jamaa muda mrefu ila hakuwa na jinsi ya kumwambia kwa kuwa si kawaida. Hence si ndo tuko likely kuwa desperate
Ni sie mwaya
 

ni age gani ikifika mwanamke anakuwa desperate?
 
inategemea ni nani mhitaji zaidi na hii kutokana na watu wanaokuzunguka
 
Umri unatofautiana tokana na mhusika. Kuna watu hata wakifika 25 wanakata tamaa. Mi niliolewa na 29 and I was not even thinking of marriage by then; but he proposed. Kwa wanawake ambao hawako shule umri unashuka. Ukiwa shule mawazo ya kuolewa yanakuwa sio kiivyo. Na pia inategemea jamii inayokuzunguka. Mi mfano ndugu zangu wote japo wameoa na kuolewa ni wale ambao hawaamini kuwa kuolewa ni lazima. Wengine mpaka walikuwa wananambia unakimbilia nini kuolewa and I was 29 imagine!

ni age gani ikifika mwanamke anakuwa desperate?
 


nimeuliza coz nadhani ningekuwa bado ningeanza ku concetrate kwenye mambo ya ndoa nikiwa 30.....blue...inategemeana, mie nilichukuliwa nikiwa bado skul.
 
Kuwa desperate ni dalili unategemea jamii ipange maisha yako... Yeyote anayetegemea jamii ipange maisha yake atakuwa desperate either Mwanamke au mwanaume..kwani atakuwa anaogopa jamii inayomzunguka itakuwa na mawazo mabaya juu yake kama aja oa au kuolewa.

Hivy basi kuwa desperate ni mawazo yako bila kujali wewe ni mwanaume au mwanamke!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…