Nani analihujumu Taifa? Tusipozinduka sasa...

Na wale waliopaswa kutoa elimu zaidi kwa raia.
Waliopaswa kuipigia CCM kelele kwa madhila wayowaona wao.

Hawafanyi hivyo na badala yake wamebaki kupiga kelele ya Katiba ambayo itawahakikishia usafi wa njia ya kuingia kwenye ulaji kwa zamu.
 
Hili hapa lingine akili ndogo na ubongo wa VIRAKA....nyie ndo kwenye bar hutole mimacho watu wanaokunywa Windhoek eti wanywe MAPUYA ili muwe sana....
Na hili hapa lingine linalotetea upigaji wa kijasusi kama ule aliojaribu Lissu na ukamshinda kwa mtindo wa MIGA na Ndege kukamatwa.

Uzawa wa kipigaji huwa haubatizwi.
commonmwananchi
10101.
 
Hayo mambo mengine ya hizo nchi unaweza ukasemea ata wewe,mwenzako mwenye akili timamu kaamua kutolea mifano ya nchi zingine kwenye ilo eneo la ujasusi wa kiuchumi ambalo ni tatizo nchini kwetu,sasa wewe badala uje na mawazo mazuri ya nini kifanyike ili nchi iweze kupiga hatua badala yake unakuja na mambo ya ovyo.Au wewe unaona ni sawa hii nchi kua hivi ilivyo?Tumia akili zako vizuri basi.
 
Kazi za BALOZI huko nje ni nini? Kwahiyo wao hawaoni fursa za kiuchumi, hawana uelewa ni kula mishahara tu basi.Kama ndio hivyo wabadilishiwe majukumu yao au wapelekwe watu wenye uelewa na mambo ya uchumi ili kushawishi wawekezaji kuja nchini.
Je!
Mleta bandiko amewahi kuisaidia nini Chadema kiushauri kama jasusi na kada mtiifu.

Mbona anawaacha viongozi wake wakifoka foka majukwaani bila sera zaidi ya Piiipoooziii!

Hatuwaoni wakisimama kidete kuipinga CCM kwa hoja na sera.

Badala yake ni kudandia matukio kila uchao na kujadili watu binafsi huku wakiwaombea vifo opponents wao!
 
Hizo nchi anazozitaja umewahi kukanyaga ardhi yake wewe binafsi?

Je umejaribu hata kwenda huko mitandaoni na kutembelea hizo nchi na ukajiridhisha kwamba wananchi wake wana Furaha kuliko Tanzania?

Mimi ninasema kile ninachokiamini.

Sifuati mtu sababu ya itikadi.
Ukisema uhalisia nitakuelewa.
Hata ukienda hizo nchi nao wanatamani ya Tanzania [emoji1241]
 
Kweli kabisa, wanadhani wakiwapa uraia pacha watakuja kuwanyang'anya nafasi za uongozi watoto wao waliopo mashuleni !! Mawazo mgando !!!
 
Hayo magari yako wapi?? Mbona barabarani mwanzo mwisho ni Yutong?

NB: Siku tukikoma kuijenga na kuiimarisha ccm tutafika mbali sana kama taifa!
Na pia mpaka tukiacha kuzishabikia klabu za Simba na Yanga nchi nzima ndio tutapata akili nzuri!! Maana ushabiki wa aina hiyo umeshaingia mpaka kwenye vyama vya siasa ! Leo hii MTU akitoa mawazo mbadala kwa yale yanayotendeka utaona MTU mwingine anamponda huyo kwa maneno kwamba eti anasema hivyo kwa sababu ni wa kutoka chama Fulani !! Hii sio akili nzuri kudhani kila anayepinga jambo Fulani eti ametoka chama Fulani ! Na kila anayesifia jambo Fulani ni lazima wa kutoka chama Fulani !! Nadhani inabidi tubadilike sio kila kitu katika nchi tukichukulie kama tunavyozichukulia Yanga na Simba !!
 
Kweli sikio la kufa halisikii dawa.Tulikuwa na Mangula Mechanical Tools (MMT)ilikuwa karakana kubwa kuliko zote kusini mwa jangwa la Sahara iliojengwa na China ya Mao.Ilikuwa na uwezo wa kuunda hata kifaru cha jeshi tokea kwenye udongo wa chuma hadi finishing.
Kwa ujinga wetu tuliuza na hakuna kitu tena pale.
Si hiyo tu karakana kubwa zilizokuwa UFI,TAZARA,URAFIKI,zimetekezwa.
Nchi yetu iliokuwa na nyenzo za kukuza uchumi wa viwanda imebakia kuwa nchi ya wafokaji wa musiki kizazi kipya.
R.I.P Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa.
 
Hilo la Bagamoyo labda kama viongozi wanasema uwongo...Tatizo kubwa la nchi yetu ni maslahi binafsi kwanza, mradi ungeweza kuwa mzuri but who are the beneficiaries? Unakuta hivyo vi percent wanavyopewa ili wawe brokers ndiyo tatizo na kuishia kutuletea mikataba ya kinyonyaji badala ya kuleta maendeleo. Ni bora hiyo miradi imehujumiwa kwasababu wanahujumiana wao kwa wao kwa maslahi yao binafsi na wala siyo kwamba taifa lina hujumiwa. Taifa lingehujumika zaidi kama miradi hiyo inge take off ikanyonya watanzania badala ya kuwanufaisha ikiwaacha nje kama watazamaji kama ilivyo kwenye madini.
 
Kujua mambo ya nchi sio lazima ukanyage.Kwasababu hata ukikanyaga bado huwezi kuyajua yote.sisi kama nchi jukumu letu nikujikita kwenye mambo ya msingi yatakayolisaidia taifa letu.Sasa wewe inaonekana bado uko kwenye akili zakuwaza vyama badala ya nchi.Ndo maana badala ujadili mada unamjadili mtoa mada kwakumhusisha na chama cha siasa cha upinzani.Sasa hayo ni mambo yaovyo.
 
Kwa hiyo bandiko nililo mjibu wewe umeokota Chadema tu?

Na hilo tu ndio limekuudhi zaidi?

Kweli bado kazi tunayo.
Mimi huwa nalumbana kwa hoja ya mada husika hivyo turudi kule.

Huyu Yericko ameandika lawama zaidi tena kwa kuilaumu historia.

Yeye angejikita kukosoa na kuleta way Forward bila haja ya lugha kejeli zisizo na tija.
 
Story zako za ujasusi ni kama za Dj Mafie.
Upupu mtupu.
 
Viwanda vingine kama mwatex, mutex, Tanganyika packers, bora shoes, kiwanda cha magunia Moro , machine tools, general tyres, sunguratex, doublecola, minjingu stamico, to mention the few kweli R.I.P Mwalimu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…