Nani analihujumu Taifa? Tusipozinduka sasa...

kupanga ni kuchagua--kama Taifa tunavyo vipaumbele kumbuka kila jambo lina wakati wake,,utafika wakati yote unayoyaona yanachelewa ..tutakuwa nayo na wakati huo ujao yataongelewa mengine.
 
Huenda unao mpango wako mwingine wa kuandika kitabu, na maandishi marefu kama haya unayaleta hapa ili yajadiliwe ili uongeze nyama kwenye hoja zako.

Maandishi yanapokuwa marefu hivi, yanahitaji muda wa kusoma kwa utulivu, na kufikiri.

Hapa ni mtandaoni, watu wanapita harakaharaka. Kuna njia za kufupisha taarifa kama hizi na kuwa kamilifu zaidi kwa mtu kuelewa kinachowasilishwa.

Basi, nimesoma hadi katikati, na kuna ninayokubaliana nawe, na mengine sikubaliani nawe.

Ninalokubaliana nawe moja kwa moja ni hii dhana ya kuingiliwa na kuwekewa mapandikizi kwenye uongozi wa nchi yetu. Hatuna tena utaratibu mzuri wa kuchuja viongozi wetu wanaofaa kuongoza nchi yetu.

Huu ni udhaifu mkubwa sana, kwa sababu yote uliyoyaelezea yanaanzia hapo.

Kwa maana hiyo basi, ingefaa kujadili jambo hili muhimu hivi na pana kiasi chake, inahitaji kuwa na mada inayojitegemea na isiyovurugwa na hiyo mifano midogomidogo uliyoiweka ya maeneo unayodhani tunahujumiwa.

Mchangiaji atazungumzia Bagamoyo, na kuondoka zake, na mwingine ataleta ya kwake juu ya nyumbu, naye atagusagusa na kuondoka. Mwisho wa siku, sijui kama utakuwa umefikia lengo la mada yako, ya kukubaliana nawe au kutokubaliana nayo kuhusu uwepo wa kuhujumiwa.

Naogopa kukuchosha kusoma gazeti langu. Angalia hayo kwanza halafu tutaendelea mbele.

Lakini iwe hujuma au vinginevyo, ninakubaliana nawe sana kwamba Tanzania tumevurugika sana katika miaka hii. Tusipobadilika, tutakuwa taifa la kichekesho sana.

Ukitaka kujua tulivyogeuka na kuwa taifa la kichekesho, anzia kuangalia maProfesa wetu, na wasomi wetu kwa ujumla.
 
Reactions: Ame
YEHODAYA nadhani utakuwa umepitia hoja nyingine za Chige

Nilishangaa sana Rais JPM akizusha uongo kuhusu Bandari ya Bagamoyo! ironically kuna madudu ya Airport ya Chato, anyways hiyo ni mada nyingine tusitoke huko.
Nyie ni waji nga jpm amepambana bado kuna watu mnadhani maendeleo yatakuja kwa kuongea na kuyatamani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu voicer naunga mkono hoja zako zote kasoro pale ulipoanza kumtaja Magufuli. Utanisamehe kwa hilo. Magufuli ndiye aliyekwamisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa kuwa tu mkataba umesainiwa na Kikwete na siyo kwa ubaya wa mkataba
Kumbe ni kweli mkataba ulisainiwa? Sasa mbona mlianza Tena kusema hakuna mkataba uliosainiwa?
 
A very serious rebuttal. to the proposition..., still, we cannot deny terrible weaknesses in our governance systems.
Samahani kwa kilugha hiki, lakini nilijisikia nitumie kilugha kujieleza.
 
Viwanda vingine kama mwatex, mutex, Tanganyika packers, bora shoes, kiwanda cha magunia Moro , machine tools, general tyres, sunguratex, doublecola, minjingu stamico, to mention the few kweli R.I.P Mwalimu !
Mkuu unanijuwa mimi nani...kaa chini
 
Wako bize kujua Mbowe kalala wapi leo.
 
Mtu akiongea kitu kuhusu maendeleo ya nchi watu wanaingizia Uchadema Uccm hatar sana hii tabia sijui itaachwa lini
Ni kwa sababu Ccm ndio chanzo cha udumavu wa watanzania
 
Ahsante kwa Uzi mzuri na wenye tija kwa Taifa na rasilimali zake.

Hakika umetufumbua na kutufungua, hakika nchi yetu inachezewa kama mpira wa kona hakuna kutuliza bali ni butu butu.

Hakika ukweli mchungu
Kazi ya Yerico ni kusema. Wenye mamalaka wako njema sana kimaisha. Hayo maviwanda ya Taifa yawepo yasiwepo kwao hayana hasara
 
Huyo Yericko Nyerere ni kada mkubwa wa Chadema.
Wewe uko nyuma na hujui ya kule mbele kwenye Dash board ya gari letu.

Ni kawaida ya Chadema kusema angalieni majirani....

Kwani uongo???
Umejibu vyema mada yake, lakini umetibua kuingiza mambo ya vyama katika katika jibu lako.
Sikuona mahali popote Yericko alipotaja au kuisifia CHADEMA katika andiko lake lote. Sasa kama wewe unamjuwa kuwa ni mCHADEMA, weka pembeni uanachama wake huo, jishughulishe kujibu hoja zlizomo kwenye andiko lake.

Hapa wewe ndiye unayetaka kuharibu mjadara kwa kuufanya uwe wa vyama vya siasa.
 
Great!!! wasikusumbuwe Mkuu hao Mapopomalism
 
Zezeta hilo. Halafu linajiona lipo sawa tu kumbe kubwa jinga.
 
BRAVE MIND 🤝🤝🤝
 
Nyie ni waji nga jpm amepambana bado kuna watu mnadhani maendeleo yatakuja kwa kuongea na kuyatamani
Alisema uongo kuhusu bandari ya Bagamoyo. Soma post ya Chige utaona
Ni kama ule wa kutumia pesa za ndani leo Rais SSH kasema ni deni la JPM
Kwenda kujenga uwanja wa Kimataifa Chato haikuwa na maana
Kaua mradi wa nyumba za Kigamboni na kwenda kujenga Mbuga yake
Kadai kuna vita ya uchumi, hakuna vita yoyote

In short leo tunaangalia nyuma tunabaini mengi kama yale aliyosema Mh Mwigulu kuhu banks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…