Nani anamtumia Luhaga Mpina? Ni Seif Ali Seif wa Superdoll?

Kwa hiyo nani atumee sisi wananchi? Mtu akisema ndio ngonjera kama hizi zinatoka
 
Hoja hupingwa kwa hoja. Chukua hoja zake zipinge kwa data halafu mwisho ndipo ueleze uliyoyaeleza! Aidha kama umekopi tu, acha kutumiaka
 
Taarifa ya Mpina imeshapenya mioyoni mwa Watanganyika!! Unapoteza muda
 
Sukari huko kwenu kilo moja ni shillingi ngapi?
Mwezi wa 4 Mpwapwa kilo ya sukari ilikuwa Tsh 10,000 na sasa ni Tsh 3,000. Wananchi tunataka sukari iwepo kwa bei ya Tsh 1,800 kama ikivyokuwa kabla Magufuli hajaingilia na KUVURUGA pale mwaka 2016.

As long as availability na affordability zitakuwa guaranteed SIJALI ni nani mfaidika wa UNAOSEMWA ni UFISADI.

Waziri BASHE kamatia hapo hapo
 
Una ushahidi mkuu au umetumwa kuzima sakata la BASHE NA SUKARI
 
Rushwa ya sukari imeajiri mitandaoni vijana wapumbavu
 
Mpina kamwaga mafuta ya taa kwenye shimo la nyoka lazima wote mtoke nje kupumua kudadadadeq. Mpina kanyagia hapo hapo hadi mafisadi papa wajitokeze nje tuponde vichwa vyao
 
Ningekua ndio mimi mbunge Meneja Wa Makampuni ningekaa na kutulia natengeneza report nzuri na data za kudefend report iliyotolewa na mbunge kisha nageuza ukweli kuwa uongo naita waandishi wa habari napresent report yangu ili kuwaaminisha wananchi nilicho kiandaa kisha naenda bungeni na report yangu napresent kwa heshima zote kwa spika na data zangu za ushahidi na bunge linakubali na kupiga makofi.
Baada ya break namtafuta mbunge mpina tunaendelea kupiga story na kucheka huku tunakunywa chai.
 
Hoja hupingwa kwa hoja. Chukua hoja zake zipinge kwa data halafu mwisho ndipo ueleze uliyoyaeleza! Aidha kama umekopi tu, acha kutumiaka
Mpina ni tapeli tu, hata morogoro ametapeli ekari 1000 za wakulima, kama anajifanya anapenda wazalendo na masikini, awarudishie mashamba yao, matrekta yake yanalima mpaka kwenye milango ya wanavijiji
 
Sasa si mpaka wawe na majibu. Ni swala la muda tutasikia Mpina kalawiti yote kumtoa kwenye mstari. Katika hili wameshikwa pabaya mno.

CCM zana pekee za vita wanazotegemea ni kukuundia shutma za uonga ama kukuKolimba.
inawezekana sana sana, kama wameshakuja na huu upumbavu basi lazima watampa zengwe kubwa sana
 
Mpina ni tapeli tu, hata morogoro ametapeli ekari 1000 za wakulima, kama anajifanya anapenda wazalendo na masikini, awarudishie mashamba yao, matrekta yake yanalima mpaka kwenye milango ya wanavijiji
Hayo ya Morogoro mngojeni huko huko sasa tunamuunga mkono kwenye sakata la sukari likiisha ndiyo mumuanzishie hilo la mashamba.
 
Hoja hupingwa kwa hoja. Chukua hoja zake zipinge kwa data halafu mwisho ndipo ueleze uliyoyaeleza! Aidha kama umekopi tu, acha kutumiaka
Kwanini usianze wewe kujibu hoja za post hii?
 
Inasikitisha sana. Hii story hapo juu nimesoma yote, hamna hata reference moja; mwandishi amejikita kumkandia Mpina. Mpina Katika andiko lake ameeleza viszuri sana kisheria na reference zipo. Huyu mweandishi ni kama simba aliyejeluiwa; Mpina kawatisha sana, sasa wanatafuta kila njia kum "character assassinate" na kwa akili ya waTanzania wanaweza kufanikiwa. Kila ukiangalia hakuna hata chembe ya ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…