Nani anamtumia Luhaga Mpina? Ni Seif Ali Seif wa Superdoll?

Hukujitambulisha andiko hili limeletwa kwa niaba ya nani.
Nani mwenye maslahi aliyogusa Luhaga Mpina?

Nikushukuru kwa hili andiko lako, kwa sababu linaongeza mwanga kwetu kuelewa nani yupo nyuma ya uchafu ambao kundi la Luhaga (kama lipo) linapambana naye.

Ni wazi hili kundi la pili halina manufaa yoyote kwa waTanzania; kama lisilo kuwa nalo kundi la upande wa pili.

Hata hivyo, waTanzania watamshukuru Luhaga Mpina, bila kujali hizo shutuma za kundi pinzani, kwa kusimama na kuyaleta nje makundi haya ili tujue adui wetu mkubwa hasa ni nani.

Kwa kusoma tu andiko lote hili la kumshutumu Luhaga Mpina, ni wazi kabisa kwamba kundi hili la upande huu halina chochote cha kuwasaidia waTanzania.
Tutaendelea kumuunga mkono Luhaga Mpina.
 
Stori stori
Mpina fanya kazi ya utume
Kama naye ana mapungufu au makosa mpelekeni mahakamani msisubiri aibue mambo ndio mseme madhambi yake
Huyo sijui kimti asifikiri yeye ndiye pekee anaijua Tz kuliko wananchi wengine.
Mnakera kwa ufupi
 
Kwani Wizi na ufisadi ndo umejenga chama? Uhaba wa Sukari ndo msingi wa chama? Tufafanulie
Sijui umelenga nini na hili swali lako, mkuu 'figga'; kwa sababu ni wazi kabisa Chama hakiwezi kuwa imara kama wizi/ufisadi unashamiri chini ya chama. Huenda hukuelewa hayo maneno machache aliyo andika huyo uliyemjibu.

CCM katika hali hii iliyopo sasa, huwezi kuiita ni CCM imara kwa kigezo cha aina yoyote.
 
Kumtafuta mwanasiasa msafi ndani ya ccm ni sawa na kutafuta bikra wodi ya wazazi, kama jinsi ambavyo yeye alitoa ushahidi wa tuhuma zake dhidi ya msomali ndivyo pia ushahidi unapaswa kutolewa dhidi yake, hizo habari za kutuambia Magufuli alipewa hekari sijui ngapi na nani na wakati alikua na uwezo kujigawia tuu kibabe naona kama ushuzi mtupu tuu
 
Wodi ya wazazi mbona bikra zimejazana tu au hao watoto wachanga wa kike hawana bikra??
 
spinning ya kishamba kabisa. Watu wana akili na wanaelewa. Hicho kikundi kinachojiita kigogo kiko kwenye pumzi ya mwisho kabisa. Kitaondoka pamoja na huyu mama wa kizanzibari soon
 
Kama hayo yanajulikana kwa uwazi kiasi hicho, kwanini serikali imeacha mambo yote hayo yatendeke bila wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria?

Huyo kigogo na kundi lake, kabla ya kuja na hizi ngonjera kwanza jibuni hoja za Mpina.
 
Baada ya kusoma hili Bango nimeanza kumdharau Mpina kumbe ni wale wale.
Hivi akili yako inachotwa kirahisi hivyo, au unayo maana yako nyingine?

Wakati mwingine utani utani kwenye maswala mazito kama haya siyo jambo zuri.

Haya, hebu tueleze heshima yako umeihamishia kundi gani?
 
Mleta mada hujawahi kuwa na akili, uchawa umekupofua macho na akili hata kama hilo andiko la hovyo umelitoa kwa kigogo, kama ungekuwa na akili timamu ungetakiwa kuliacha huko huko.
 
Jamani watanzania nani katuloga?
Hivi kila anayeleta hoja nzito kuibua uozo unaoligharimu taifa letu tunamuona katumwa?
Nini maana ya mtu kuwa mwakilishi wa wananchi?

''Kiongozi mmoja vya chombo cha dola aliposema,wapo waamiaji haramu wameingia kwenye siasa tena
wana nafasi za juu'',sikumuelewa,lakini baada ya hoja ya mbunge Mpina ambayo ni nzito,nimeelewa
Ila kwa akili hii ya kudhani katumwa,basi tuendelee kunawa mikono kwa maji tiririka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…