Nani anamwelewa Mhe. Rais anatupeleka wapi?

Nani anamwelewa Mhe. Rais anatupeleka wapi?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mimi Kwa maoni yangu namwona Mhe. Rais akitupeleka kuyafikia haya yafuatayo;
1. Taafa lenye maridhiano ambalo litatufanya sote tuwe ndugu

2. Anaelekea kutuachia Taifa lenye Katiba mpya itakayoratibu maendeleo na ustawi wetu kulingana na mahitaji ya sasa

3. Upo uwezekano mkubwa akatuachia Taifa lenye utofauti mkubwa Kati ya mwenye nacho na asiye nacho. Hii nikutokana na ukweli kwamba nafasi nyingi anazotoa za kiutawala azizingatii uwezo Bali zinazingatia unatoka familia gani, unafahamiana na Nani na uliteseka kiasi gani huko nyuma.

4. Kiwango cha rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kitaongezeka Kwa Kasi katika kipindi chake Kwa Sababu; viongozi waandamizi wote wanazinguka kujustify posho huku Ofisi zikibaki Bila watoa maamuzi. Hakuna anayecontrol safari za viongozi, hakuna anayepima tija ya safari na hakuna anayefuatilia matumizi ya fedha za serikali zinazotumiwa na viongozi. Ongezeko kubwa la Kula urefu wa kama linamomonyoa kabisa fedha za kuendeleza umma.

5. Upo uwezekano mkubwa Mhe. Rais kufikia 2025 au 2030 incase alishinda uchaguzi; tukawa na watu wengi wasiojiamini ( wanafiki). Wakati wa JPM walizaliwa watu wakupongeza kila linalofanywa, tulitegemea awamu hii watu hawa wapungue lakini wanaongezeka na baadhi wameamua kujipachika title ya chawa. Tanzania siyo kisiwa, tupo kwenye ushindani mkubwa WA kiuchumi Duniani, lakini pia Dunia IPO kwenye vita ya uchumi inayochangiwa na scarcity ya resources. Katika ulimwengu huu WA ushindani, chawa Hana nafsi katika issue serious. Ongezeko la chawa linatuondoa kabisa katika ushindani nje ya mipaka yetu; ikumbukwe kwamba tunaweza tukadanganyana ndani lakini nivigumu kudanganya Dunia.

6. Upo uwezekano mkubwa Mhe. Rais akatuachia taasisi imara kwenye vitabu hasa ikizingatiwa kwamba anakwenda kutupa katiba mpya; pamoja na taasisi imara kimuundo ufanisi unaweza ukawa mdogo Kwa Sababu hakutakuwa na rasilimali watu yenye uwezo na karba ya kusimamia taasisi hizo imara.

7. Upo uwezekano mkubwa Mhe. Rais akalazimika kuajiri watendaji WA juu kutoka nje ambao NI Watanzania na wasio Watanzania pale atakapoona na kuamini kwamba uchawa umefeli. Mhe. Rais wa Zanzibar ameanza huu Mkakati, most of senior officers WA serikali ya Mwinyi amewatoa ughaibuni (Diaspora), hii NI baada ya kuona Zanzibar hakuna watumishi serious. Matokeo yake mishahara watakayolipwa hawa Diasporas haitakuwa wanayolipwa wazawa, wao watakuja kutoka makampuni serious na package zao NI kubwa; Kwa mantiki hiyo wage bill itapanda Sana na hivyo uchumi kukosa ustahimilivu. Katika eneo hili tukubaliane kwamba Mhe. Rais anapaswa kutafuta vipaji kwenye secta za ndani mapema kabla wateule wake awajamkandamiza na ngonjera za anaupiga mwingi.

8. Kadri miaka inavyosonga, upo uwezekano nguvu kubwa ya serikali yake ikakimbilia kwenye vyombo vya habari kuteka maudhui ili abaki kusifiwa yeye Tu; kelele za kudorora Kwa uchumi zitawapelekea wasaidizi wake kuchukua fedha na kuzotumia zaidi kwenye uhabarishaji kuficha hoja na njaa za wananchi. JPM alifanya haya lakini baada Tu yakuondoka hata TBC ilibadili maudhui ya vipindi vyake ikaacha kuimba juhudi.

Nini kifanyike kumsaidia Mhe. Rais asikwame katika kuwasaidia wananchi?
1. Asikubali kuelekezwa Aina ya katiba wanayotaka wananchi; aruhusu mchakato huru tuona value for money.

2. Atengeneze mfumo wa kielekronikia wa malipo ya posho za safari na matumizi ya viongozi utakaoondoa mamlaka yakuidhinisha fedha cash kwenye taasisi nyingi. Hii itasaidia kufanya udhibiti wa fedha zinazotumiwa na watu wachache na itawalazimisha viongozi kuumiza vichwa wafanye safari zenye tija. Lakini pia mfumo huu ambao yeye anaweza kuwa msimamizi mkuu utampa picha halisi ya matumizi ya viongozi baina ya sekta Bila kulazimika kuomba taarifa popote. Nchi zilizoendelea kila shillingi Inayotolewa inasomeka kwenye akaunti ya mlipwaji.

3. Akubali kuachana na upendeleo katika uteuzi; teuzi zifanyike Kwa merits na adhibiti kabisa kuteua viongozi nje ya taasisi husika. Wapo watu wanasota kwenye utumishi WA umma na wanafanya KAZI Kwa uadilifu lakini wakifika nafasi za juu wanaletewa MTU mwingine kabisa na hivyo wanavunjika moyo kufanya KAZI.

4. Awatengeneze viongozi wanaojiamini ndani na nje ya nchi.

5. Aepuke mapumizi makubwa ya watu kutoka nje wakiwemo Diasporas katika nafasi za juu za utawala; kuendelea kutegemea wageni kutoka nje ya sekta nikutengeneza mgomo baridi ndani ya sekta husika.

6. Kwa kuwa Mama NI mcha Mungu, azidi kumwomba Mungu ampe upeo wakuendelea kutambua kuwa cheo NI dhamana na kwamba WATANZANIA NI zaidi ya CCM,

Kila la kheri
 
1. Asikubali kuelekezwa Aina ya katiba wanayotaka wananchi; aruhusu mchakato huru tuona value for money.
Hili umefeli absolutely! Katiba hatengenezi au haitegenezwi katiba kwa hisani na maelekezo yake, katiba ni ya wananchi. Warioba Katiba draft contains peoples wishes!

Yaliyobaki umeyaeleza vizuri kabisa and agreed
 
Hapo dawa pekee ni kuiondoa tu ccm madarakani. Maana ndiyo chanzo cha hayo madudu yote uliyo yataja.

Kinyume na hapo, hakuna hata takwa lako moja hapo litakalo tekelezwa kwa usahihi.
 
Ukimtaja JPM kwa kudhihaki hutaeleweka sababu kazi zake zipo kila mahali. Anzia tu hapo nyumbani kwako kwenye huduma ya maji, umeme na ulinzi enzi za JPM.
 
Hili umefeli absolutely! Katiba hatengenezi au haitegenezwi katiba kwa hisani na maelekezo yake, katiba ni ya wananchi. Warioba Katiba draft contains peoples wishes!

Yaliyobaki umeyaeleza vizuri kabisa and agreed
Ndo maana nimesema asisikilize watu wanaomzunguka asikilize wananchi katika mjadala huru
 
Back
Top Bottom