JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Chanjo za COVID-19 ziko salama kwa watu wengi wenye umri wa miaka 18 na zaidi, na hata wale wenye changamoto za kiafya kama vile shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari, pumu, magonjwa ya mapafu, ini figo pamoja na mengineyo.
Inashauriwa kuwa endapo kuna ufinyu wa chanjo katika eneo lako, ni vema kujadili hali yako na mtoa huduma ikiwa:
- Una kinga ya mwili iliyoathirika/dhoofika
- Una ujamzito (ikiwa unanyonyesha, unapaswa kuendelea baada ya chanjo)
- Una historia ya mzio (allergy), hasa kwa chanjo au viambatanishi vyake
- Unajijua kuwa ni dhaifu sana
Kikundi cha Ushauri cha Wataalam wa Kimkakati (SAGE) cha Shirika la Afya duniani (WHO) kimehitimisha kuwa chanjo ya Pfizer / BionTech inafaa kutumiwa na watu wenye umri wa miaka 12 na zaidi. Watoto wenye umri kati ya miaka 12 na 15 walio katika hatari kubwa wanaweza kupewa chanjo hii pamoja na makundi mengine yanayopaswa kupewa kipaumbele kwenye chanjo.
Hata hivyo, Majaribio ya chanjo kwa watoto yanaendelea na WHO itasasisha mapendekezo yake.
Chanzo: WHO