Nani anapaswa kupiga goti wakati wa kuvishana pete ya uchumba?

Nani anapaswa kupiga goti wakati wa kuvishana pete ya uchumba?

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
kwenye picha nyingi za uchumba, , tunaona mwanaume akipiga goti moja huku akimvisha mwanamke pete. Hii imekuwa desturi inayotambulika katika tamaduni za Kimagharibi, ambapo kupiga goti huhusishwa na heshima, upendo na kujitoa kwa mwenza.

Lakini kizazi cha sasa kinaanza kuhoji: kwa nini iwe mwanaume pekee anayepaswa kupiga goti? Ikiwa wote wameamua kuoana na pete ni ishara ya ahadi ya pande mbili, kuna wanaoona hakuna tatizo mwanamke naye kupiga goti au hata wote kupiga magoti. Hata katika miaka ya hivi karibuni, wanawake wamekuwa wakifanya proposals kwa wanaume, jambo linalozua mjadala kuhusu kama desturi hii bado inapaswa kuwa na kanuni za kijinsia.

Sasa wewe unaonaje? Mwanaume ndiye anayepaswa kupiga goti kwa sababu yeye ndiye anayefanya proposal, au katika dunia ya usawa wa mahusiano mwanamke anaweza pia kupiga goti? Na kama mwanamke ndiye aliyenunua pete na kumuomba mwanaume wafunge ndoa, nani apige goti?

1786967321414.png
 
Yeyote tu. Ama msifanye kabisa.

Sidhani kama kuna kipengele cha bibilia/quran kinacholazimisha hilo jambo.
 
Mwanaume. Mkiiga tamaduni za watu msijitie ujuaji. Unless mbaki na zenu ambazo hazina hayo mambo.
 
Back
Top Bottom