Nani anastahili salam ya shikamoo?

Nani anastahili salam ya shikamoo?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mwaka 2010, nilienda na rafiki yangu nyumbani kwao Usukumani. Nilishangaa nilipoamkiwa "shikamoo" na dada yake ambaye alionekana wazi anaweza akawa mkubwa kwangu. Ndivyo alivyoniamkia na ndivyo alivyomsalimia pia rafiki yangu ambaye ni ndugu yake wa damu.

Japo niliitikia, lakini ilikuwa kwa shingo upande. Sikuwa na uhakika kama nilistahili au la. Nilifikiri kakosea. Lakini siku chache baadaye, nilikuja kugundua kuwa hakusalimia kimakosa. Alijua alichokiwa anakifanya.

Alikuwa ni mkubwa kiumri kwa rafiki yangu ambaye ni ndugu yake, na alijua hilo lakini bado alimwamkia. Nilikuja kubaini kuwa kwa utamaduni wao, mwanaume ni mkubwa kwa mwanamke hata kama ni mdogo kiumri. Kwa hiyo ni kawaida kwa dada mtu kumwamkia "shikamoo" mdogo wake wa kiume.

Kwetu sisi, mkubwa ndiye anayeamkiwa hivyo.

Sijawahi kukutana na changamoto ninayotaka kushirikisha, lakini natamani kufahamu.

Inajulikana kuwa kwa tamaduni za baadhi ya makabila, ni kawaida kwa baadhi ya wazee kuoa wake zaidi ya mmoja, na wakati mwingi anaweza akaoa mwanamke anayelingana na mtoto wake wa kumzaa na hata mdogo zaidi.

Sasa chukulia, kwa mfano, baba mtu kaoa binti aliyesoma darasa moja na mtoto wake! Huyo mtoto atamsalimiaje mke mdogo wa baba yake?

Ikumbukwe kuwa mke wa baba mtu ni "mama" mtu pia.

1. Atamwita mama hata kama walikuwa marafiki shuleni na wanalingana umri?

2. Atamsalimia "shikamoo mama"?
 
Hii kitu sidhani kama bado ipo labda huko ndani kabisa. Kingine wasukuma ni waoga by nature
Kivipi mkuu? Kwa vile mwanamke humwamkia mdogo wake wa kiume "shikamoo"?

Sidhani kama huo ni uoga. Ni utamaduni wao. Ila sijaenda huko muda mrefu hivyo sijui kama wangali wana hiyo desturi.
 
Swali gani hilo?

Yaani mke wa bab'ako unahitaji kujali umri wake kabla umsalimie?
 
 
Binafsi hiyo salamu naichukia sana.
 
Swali gani hilo?

Yaani mke wa bab'ako unahitaji kujali umri wake kabla umsalimie?
Tuelimishane mkuu! Hakuna anayejua kila kitu.

Chukulia baba yako kamwoa binti uliyesoma naye darasa moja, tena ambaye umemzidi kidogo umri, labda kwa miaka mitatu, utamsalimiaje?

1. Shikamoo mama?
2. Habari?
 
Mnapo ambiwa tamaduni za kitanzania sio kukataa ushoga pekee, nipamoja na hizo mkuu.

Mke wa baba unampa heshima Kama mke wa baba ako ata Kama umemzidi umri.

Kila kabila Tanzania Lina tamaduni zake.

Wasukuma, na sisi pia hua hatuwasalimii Dada zetu.

Dada angu ananipa heshima Kama kaka ake at Kama aliwahi kuzaliwa nami Nampa heshima Kama Dada angu.

Ila tukisalimiana ki kabila ndo inaeleweka vizuri.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom